HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 13, 2022

WAGAWA MAHITAJI KWA VITUO VINNE VYA WATOTO YATIMA ZANZIBAR.


Na.Khadija Seif, Michuzi TV

JAMII imetakiwa kuwaonyesha upendo watoto waishio na virusi vya ukimwi Ili kujiona wenye thamani na Haki ya kuishi na kuyafikia Malengo yao kama watoto wengine.

Akizungumza hayo Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima wanaoishi na virusi vya ukimwi kilichopo fuoni Visiwani Zanzibar ,Abdul Majid amesema wakati mwengine watoto hao wanachohitaji kwenye jamii ni upendo na Mapenzi.

"Jamii haitakiwi kunyanyapaa watoto Hawa kwani bado Wana Haki ya kuishi na Wana Haki ya kupendwa na kutimiza Malengo yao kama watoto wengine."

Hata hivyo ametoa shukrani Kwa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) Kwa kufika kituoni hapo na kugawa baadhi ya Mahitaji Kwa lengo la kusaidia watoto hao .

Kwa upande wake Meneja wa Shirika hilo Hamida Juma ametoa pongezi za dhati Kwa wizara ya Maendeleo, jinsia na watoto kwa upande wa Visiwani Zanzibar kwa kuwashika Mkono bega Kwa bega na kuhakikisha wanatoa misaada Kwa vituo vya watoto yatima vinne.

Meneja wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) Hamida Juma akiwa na viongozi wa Shirika hilo pamoja na watoto yatima kutoka kituo kilichopo fuoni Visiwani Zanzibar mara baada ya kupokea Mahitaji mbalimbali ikiwemo Mchele,Sabuni,Mafuta na Sukari vilivyotolewa na Shirika hilo



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad