HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 13, 2022

BENKI YA NMB YASHIRIKI HAFLA UWEKAJI JIWE LA MSINGI AWAMU YA TATU UJENZI WA RELI KUTOKA MAKUTUPORA MPAKA TABORA.

 


Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya NMB – Emmanuel Akonaay akimuelezea Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa, jinsi benki ya NMB ilivyoshiriki katika mradi wa SGR kupitia wakandarasi wa mradi huo kwanzia Dar- Morogoro, Morogora- Dodoma mpaka sasa, Makutupora- Tabora. Pia, namna benki ilivyowawezesha wazabuni wa mradi huo kwa kuwapa mitaji na kuhakikisha watumishi wanalipwa kupitia Benki ya NMB.Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Sospeter Magesse(kulia), akizungumza na wajasiliamali ambao ni wateja wa NMB waliofika katika viwanja vya Cheyo B, Tabora kwa ajili ya kuuza na kuonesha bidhaa zao ambao pia wengi ni wazabuni katika mradi wa SGR.Wateja wa NMB wakipata huduma mbalimbali katika banda la benki hiyo katika viwanja vya Cheyo B.




***********************

Kama ilivyokuwa katika miradi mbalimbali ya kimkakati, Benki ya NMB imeendelea kuwa mstari wa mbele kwenye kutoa ushirikiano kwa Serikali na Wakandarasi ili kuhakikisha miradi inayojengwa kwa manufaa ya Watanzania inakamilika kwa wakati.

Katika mradi wa reli ya kisasa ya SGR, Benki ya NMB imeshiriki katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika awamu ya tatu ya ujenzi wa reli hiyo yenye urefu wa kilomita 368 kutoka Makutupora mpaka Tabora. Mbali na kuwa wabia katika mradi huu mkubwa, benki hiyo imedhamini shughuli hii ya uwekaji wa jiwe la msingi iliofanyika katika viwanja vya Cheyo B, Tabora.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad