HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 21, 2022

MKAZI WA MBAGALA SAIDA CHITIME AJIZOLEA MAMILIONI YA BIKO

 
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Mkazi wa Mbagala, jijini Dar es Salaam, Saida Chitime, amefanikiwa kushinda sh Milioni 10 kutoka kwenye droo kubwa ya Biko iliyochezeshwa Sikukuu ya Pasaka na kukabidhiwa fedha zake jana jijini hapa.

Akizungumza katika makabidhiano ya fedha zake, Sauda aliishukuru Biko kwa kumkabidhi fedha zitakazoweza kubadilisha maisha yake, akiamini kuwa mchezo huo ni fursa nzuri kwa Watanzania wote wenye nia ya kuondoka kwenye mkwamo kimaisha.

Alisema fedha hizo atazitumia vizuri ikiwa ni pamoja na kuanzisha ujenzi wa nyumba yao iliyokwama kwa siku nyingi kutokana na kukosa pesa, licha ya kumiliki kiwanja jijini Dar es Salaam, huku akisema ni rahisi kucheza Biko kwa kuingia live www.biko.co.tz au kwa namba ya Kampuni 505050 na 2456 namba ya kumbukumbu.

"Biko ni mchezo ambao nimekuwa nikiona watu wanashinda, hivyo nikaamua kuingia kucheza ili nishide kama wenzangu jambo ambalo Mungu amenisaidia leo kukabidhiwa pesa hizi. Nawaomba Watanzania wote wacheze Biko ili nao wajibukulie zawadi za fedha," Alisema Sauda.

Mbali na wanaocheza kwa kupitia www.biko.co.tz, pia wanaotumia simu za kawaida nao wataendelea kucheza kama zamani kwa kutumia namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu namba 2456 na wote kujishindia kuanzia sh 2500 hadi milioni tano papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa zinazofanyika kila Jumapili.Mkazi wa Mbagala, jijini Dar es Salaam, anayejulikana kwa jina la Saida Chitime katikati, akiwa mwenye furaha kubwa baada ya kukabidhiwa fedha zake Sh Milioni 10 alizoshinda kwenye droo kubwa ya Biko iliyochezeshwa Jumapili iliyopita. Kushoto ni Balozi wa Biko Kajala Masanja akiwa na Samia Karimu, Meneja Uhusiano wa Bank ya CRDB Tawi la Premier lililopo Palm Beach, Dar es Ssalaam. Picha na Mpiga Picha Wetu.Meneja Uhusiano wa Bank ya CRDB tawi la Premier lililopo Palm Beach, Dar es Salaam, Samia Karim, akiwa na mshindi wa Milioni 10 wa Biko, Saida Chitime, mwenye maskani yake Mbagala, Jijini Dar es Salaam wakati anamkabidhi fedha hizo tayari kuziingiza kwenye matumizi yake. Picha na Mpiga Picha Wetu.


Balozi wa Biko Kajala Masanja akionyesha pozi na tabasamu pana wakati anamkabidhi fedha zake Sh Milioni 10 mshindi wao wa Mbagala, Saida Chitime, alizoshinda mwishoni mwa wiki. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad