HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 21, 2022

KAMPUNI YA VIVO ENERGY YATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA 'JAZA USHINDE'

KAMPUNI ya Vivo Energy Tanzania inayosambaza na kuuza mafuta yenye chapa ya Engen nchini leo imewatambua na kuwazawadia washindi wawili kutoka mkoa wa Dar es Salaam walioshiriki kampeni hiyo iliyopewa jina la Jaza Ushinde na Engen.

Washindi hao ni Bw.Peter Assanga kutoka kampuni ya Travel Partners aliyejishindia TV ya flat screen na Bw.Kassim Moto dereva wa bajaj maeneo ya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam aliyejishindia friji. Jaza Ushinde na Engen ilitaka kuwashukuru na kuwazawadia wateja wao kwa kila ununuzi wa mafuta katika vituo vyao vya huduma nchini kote. Ofa hiyo ya wiki nane itafungwa tarehe 9 Mei 2022. Mbinu ya kuingia kwenye ofa itakuwa kupitia droo ya bahati nasibu. Ambapo wateja watapokea kuponi wanaponunua petroli au dizeli

Wateja wanatakiwa kujaza kuponi hizo, kuambatisha nakala ya risiti ya malipo na kuingiza kwenye kisanduku cha bahati nasibu ndani ya kituo, na kuondoka na kuponi ili iweze kutumika kama kithibitishwa ikiwa utawasiliana naye kama atabahatika kuwa mshindi.
Kutakuwa na droo mbili kila mwezi. Ambapo awamu ya kwanza ya washindi watajishindia Fridges na TV na droo nyingine kuu mwezi Mei, ambapo washindi watajishindia aidha Pikipiki za Boxer BM125, Fridges, TV Flat Screen au zawadi nyingine nyingi.
Afisa wa kampuni ya Travel Partners Bw.Peter Assanga aliyejishindia TV ya flat screen baada ya kushiriki katika shindano la Jaza na Ushinde linalofanyika na kampuni ya Engen Tanzania mapema leo pale Mwembeyanga. Katika hafla ya makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Serikali ya Mtaa Bw.Shabaan Mtuya (kushoto), Bw.Emmanuel Singilimo, Meneja wa Fedha wa Kampuni ya Engen Tanzania na kulia kabisa, Bi.Fatma Hassan ambaye ni Mkurugenzi wa biashara hiyo iliyopo Ubungo.
Mshindi wa friji katika shindano la 'Jaza na Ushinde' Bw.Kassim Moto (katikati) akiwa amesimama kwa furaha pamoja na Mkurugenzi wa Serikali ya mtaa wa Temeke Bw. Shabaan Mtuya (kushoto) Bw. Emmanuel Singilimo Meneja wa Fedha wa Kampuni ya Engen. Tanzania, Bi Hellen Kileo, Meneja wa Kituo cha Petroli cha Engen kilichopo Mwembeyanga na Bw. Suleiman Sood, Meneja wa reja reja (kulia).                                                                     
Nadine Kapya: Bw Kassim Moto akiwa na wenzake baada ya kushinda friji kutoka Engen Tanzania. Bw Kassim alikuwa moja na washindi ya shindano ya Jaze Ushinde.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad