HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 19, 2022

MICHUANO YA KOMBE LA MEI MOSI 2022


Mchezaji Sophia Komba wa timu ya netiboli ya Ofisi ya Rais Ikulu (mwenye jezi ya njano) akiuwahi mpira huku Regina Mfinanga wa SHirika la Maendeleo ya Petrol nchini (TPDC) naye akijaribu kuuwahi mpira huo katika michuano ya kombe la Mei Mosi Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

 *TANESCO, TANROADS zapindua meza


Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TIMU za Shirikal la Umeme nchini (TANESCO) na timu ya wanawake ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) wamepindua meza na kukataa kufungwa na wapinzani wao katika mechi za michezo ya soka na kuvuta kamba iliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini hapa.

Katika mchezo wa soka TANESCO walipindua meza kwa kuwafunga TAMISEMI waliokuwa wakiongoza kwa bao 1-0 hadi kipindi cha kwanza kumalizika ambapo hadi mwisho wa mchezo TANESCO walifunga magoli 3-2 yaliyofungwa na Kurwa Mangara (2) na Ibrahim Salum (1), huku ya wapinzani wao yalifungwa na Lewis Mwakasega na Khamis Shedafa.

Nao TANROADS katika mchezo wa kuvuta kamba kwa wanawake walitoka sare dhidi ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwa mvuto 1-1, ambapo awali walivutwa kwenye mvuto wa kwanza. Mchezo huu umefanyika viwanja vya Jamhuri jijini hapa.

Katika mchezo wa Wizara ya Mambo ya Ndani waliwachezesha kwata kali Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kwa kuwafunga magoli 58-6. Hadi mapumziko washindi walikuwa mbele kwa magoli 28-3; wakati Uchukuzi SC waliwaadabisha Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa kuwachapa magoli 37-22. Washindi waliongoza kipindi cha kwanza kwa magoli 17-10.

Nayo timu ya Ofisi ya Rais Ikulu iliwashinda Shirika la Maendeleo ya Petrol nchini (TPDC) kwa magoli 45-6, hadi mapumziko washindi walikuwa na magoli 22-2; wakati timu ya Wakala wa Chakula nchini (NFRA) waliwafunga Wizara ya Maji kwa magoli 20-11, hadi mapumziko washindi walikuwa na magoli 8-3.

Michezo mingine iliyochezwa na matokeo yao yakiwa kwenye mabano ni Wizara ya Nishati walishinda (25) dhidi ya Chuo cha Mipango (9); Shirika la Umeme (TANESCO) (52) na Wizara ya Kilimo (11); Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) 20 dhidi ya Kongwa DC (18); UDOM (38) huku Wakala wa Barabara nchini i(TANROADS) 13; Wizara ya Mambo ya Ndani tena 53 na Wizara ya Afya 7; na TARURA (14) dhidi ya Chuo cha Mipango (12).

Katika mchezo wa kuvuta kamba kwa wanaume timu ya NCAA waliwashinda Wizara ya Maliasili na Utalii kwa 20; Chuo cha Mipango waliwavuta Wizara ya Maji 2-0; Mahakama katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa waliwashinda TPDC kwa 2-0; Uchukuzi SC waliwavuta Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa 20; nao Wizara ya Mambo ya Ndani waliwaliza Hazina kwa 2-0; wakati Wizara ya Kilimo ilipata ushindi wa chee dhidi ya TARURA waliochelewa kufika uwanjani, pia NEC walipata ushindi wa chee baada ya Ofisi ya Mkaguzi mkuu (NAOT) kutofika kiwanjani.

Kwa upande wa wanawake timu ya Uchukuzi walivuta Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo 2-0; huku Mahakama wakiwaadabisha Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kwa 2-0; NEC wakiwavuta TANESCO kwa 2-0; Hazina wakiwavuta Wizara ya Afya 2-0; Wizara ya Kilimo wakiwafurusha Wizara ya Maji kwa 2-0 ; huku TAMISEMI wakiwavuta Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa 2-0; nao TANROADS wakitoshana nguvu na Mambo ya Ndani kwa kutoka sare ya 1-1; wakati Shirika la Maendeleo ya Petrol nchini i(TPDC) wakipata ushindi wa chee baada ya TATURA kuchelewa kufika kiwanjani.

Michuano hii iliyoanza tarehe 16 April, 2022 inatarajiwa kufunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka tarehe 21 April, 2022
Timu za wanawake za Wizara ya Mambo ya Ndani (kushoto) na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) wakivutana katika mchezo wa kuvuta kamba wa michuano ya kombe la Mei Mosi Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Timu hizo zimetoka sare ya 1-1
Mshambuliaji Kurwa Mangara (kula) wa timu ya Shirikal la Umeme nchini (TANESCO) akiokoa mpira pembeni huku beki Kitwana Seleiman wa TAMISEMI akijaribu kuondosha hatari hiyo katika michuano ya kombe la Mei Mosi Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad