HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 28, 2022

GF TRUCKS - YAFUTURISHA WADAU NA WAFANYAKAZI

 


Waislamu na wanajamii kwa ujumla wametakiwa kuutumia mwezi Mtukufu wa Ramadhani kubadili tabia kwa kutenda yaliyo mema na kuyaendeleza hata baada ya kumalizika mfungo.

Rai hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni GF Truck & Equipments LTD, Mehboob Karmali mara baada ya kufuturisha wadau mbali mbali na wafanyakazi wa kampuni hiyo .

Alisema mara nyingi mwezi huo umekuwa ukileta utulivu katika jamii, “Haijalishi ni kijana, mzee, Muislamu na asiyekuwa mwislamu, ilimradi wengi hutulia na kuuheshimu, hivyo ni vema kuendeleza yale mema hata katika nyakati nyingine ili jamii iwe salama.

“Kipindi hiki pia ni vema kuwapa wahitaji sadaka kwa kile kidogo tutakachojaaliwa kwa sababu tunazidiana “alisema Karmali.Kwa upande wa mgeni mualikwa katika Iftari hiyo, Sheikh wa msikiti wa Khoja Shia Ishnashri Jamaat ya nchini Uingereza, Syed Ali Raza Rizvi aliwasihi Waislamu hususani vijana kudumisha amani na upendo baina yao.

Pia alitumia fursa hiyo kuwaasa wafanyakazi wa kampuni hiyo kufanya kazi huku wakimtanguliza Mungu ili wanapofanya maamuzi yoyote yawe kwa faida ya kazi yao na Taifa kwa ujumla.

“Ukimtanguliza Mungu katika kila jambo lazima utafanikiwa, ila ukiwajali wengine na kuwahurumia utafanya maamuzi ya busara siku zote, hivyo tuyazingatie haya ili kufikia mafanikio tunayoyakusudia”alisema Raza Rizvi.

Hii ni kawaida kampuni ya GF Trucks & Equipemnts LTD, kujumuia na wafanyakazi wake na wadau katika matukio mbalimbali ikiwamo kufuturisha pamoja na kutoa misaada kwa yatima na wasiojiweza.

 Kampuni hiyo inajishughulisha na uuzaji wa magari makubwa(trucks) na mitambo ya kutengenezea barabara.

Mkurugenzi wa kampuni ya Gf Truks & Equipment’s Ltd, Imran Karmali  akimwangalia mfanyaklazi wa kampuni, Isack Shehemba hiyo aliye jishindia Redio (saboufa) wakati wa hafla ya Iftari iliyoandaliwa na kampuni hiyo iliyofanyika jijini Dar Salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya Gf Truks & Equipments Ltd, Mehboob Karmali (kushoto)akimkaribisha Shekh wa mskiti wa Khoja Shia Ishnashri Jamaat ya nchini Uingereza Shekh, Syed Ali Raza Rizvi wakati wa hafla ya Iftari iliyoandaliwa na kampuni hiyo iliyofanyika jijini Dar Salaam.

Baadhi ya wadau na wafanyakazi wakichukua chakula
Shekh wa mskiti wa Khoja Shia Ishnashri Jamaat ya nchini Uingereza Shekh, Syed Ali Raza Rizvi akiangalia zawadi ya Tasbihi  bada ya kupewa  na  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya Gf Truks & Equipments Ltd, Mehboob Karmali wakati wa hafla ya Iftari iliyoandaliwa na kampuni hiyo iliyofanyika jijini Dar Salaam.Kushoto ni All Jawad Karmal

 Wageni waalikwa wakiwa katika Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad