Naibu
Katibu Mkuu – Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru,
akigonga kengele kama ishara ya kuorodheshwa rasmi ‘NMB Jasiri’ kwenye
Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam. Wakishuhudia ni; Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es
Salaam (DSE) – Moremi Marwa(Kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya
NMB- Ruth Zaipuna na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji
na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama (Kulia).
Naibu
Katibu Mkuu – Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru,
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji – CPA Nicodemus D. Mkama,
Mkurugenzi Mkuu wa DSE- Moremi Marwa, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya
NMB – Ruth Zaipuna, Afisa Mkuu waFedha Benki ya NMB – Juma Kimori pamoja
na wawakilishi kutoka FSD Africa, Ubalozi wa Uingereza, International
Finance Co-operation (IFC), Orbit Securities Ltd na UN Women wakiwa
katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya kuorodhesha hati fungani ya
NMB Jasiri katika Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE).
******************************
Benki
ya NMB imefunga mauzo ya Hati Fungani ya Jasiri (NMB Jasiri Bond) kwa
mafanikio makubwa Iliyoweka rekodi ya makusanyo Afrika Mashariki na Kati
ya Sh. Bil. 74.27 na kuvuka lengo la Sh. Bil. 25, ufungaji ulioenda
sambamba na kuiorodhesha rasmi hati hiyo katika Soko la Hisa la Dar es
Salaam (DSE).
Hafla hii ilihudhuriwa na Mgeni rasmi Naibu Katibu
Mkuu- Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru aliyemwakilisha
Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande, ametangaza rasmi kuorodhozeshwa kwa
hati fungani ya Jasiri na sasa kuanza kununuliwa na kuuzwa kupitia soko
la hisa la Dar es salaam.
Akizungumza Mafuru aliipongeza NMB kwa
ubunifu chanya wa Jasiri Bond, hati fungani iliyolenga kukusanya fedha
ili kutoa mikopo kwa biashara ndogo ndogo na za kati zinazo milikiwa au
kuongozwa na wanawake na biashara ambazo bidhaa au huduma zake zinamgusa
mwanamke moja kwa moja.
“Hii sio mara ya kwanza kwa NMB kuja na
Hati Fungani na kuvuka lengo la makusanyo, hii ni mara ya nne na kwa
hati hii ambayo ni ya kipekee, kama jina lake lilivyo, kumekuwa na
ujasiri mkubwa sana, kwani jina Jasiri linaashiria mambo mengi sana.
“Ujasiri
wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), ya kuiruhusu Hati
Fungani hii kuingia sokoni kabla hata ya sheria zake hazijawa tayari,
jambo linalothibitisha imani ya mamlaka hii kwa NMB ilivyokuwa kubwa.
“Lakini pia, NMB ikalenga kupata Sh. Bil. 25 na hatimaye inafunga mauzo
ikiwa imepata zaidi ya mara tatu ya lengo, hii ni kuthibitisha kwamba
kuna nguvu kubwa ya kiuchumi miongoni mwa wanawake, tunachotakiwa ni
kuweka mazingira wezeshi ya kuwaamini kama wenzetu NMB walivyofanya,”
alisisitiza Mafuru.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB,
Ruth Zaipuna, alisema NMB ilipokea maombi 1,630 yaliyowezesha kukusanya
Sh. Bil. 74.27 badala ya Bil. 25 na kuwashukuru wateja na wawekezaji
wote kwa kuiamini benki hio.
“Kuaminika kwa NMB katika hili
kunathibitishwa na kuwa asilimia 96 ya waliotuma maombi ya kununua Hati
Fungani, yamepitia katika matawi yetu, huku asilimia 4 tu yakifanyika
kupitia Madalali wa Soko la Hisa waliosajiliwa”.
Naye Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji (CMSA), Nicodemus Mkama, aliipongeza
Bodi ya Wakurugenzi na Uongozi wa NMB, kwa kufanikisha uuzwaji wa
‘Jasiri Bond’ kwa Umma wa Watanzania na hatimaye kufikia hatua ya
kuiorodhesha DSE, tayari kwa mauzo ya walionunua na manunuzi ya
waliokosa katika mchakato uliofungwa.
Wengine waliohudhuria hafla
hii ni Mkurugenzi Mkuu WA DSE, Moremi Marwa, pamoja na wawakilishi
kutoka FSD Africa, Ubalozi wa Uingereza, International Finance
Co-operation (IFC), UN Women na Orbit Securities Ltd.
Thursday, April 28, 2022

BENKI YA NMB YAKUSANYA BIL. 74.3 KUPITIA HATI FUNGANI YA ‘NMB JASIRI’
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment