HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 6, 2022

Benki ya NBC imezindua Kampeni ya ‘Jaza Kibubu Tusepe’

 


BENKI ya NBC imezindua Kampeni ya ‘Jaza Kibubu Tusepe’ itakayojikita kwenye utoaji wa elimu kwenye masuala ya kifedha itakayoambatana na zawadi chungumzima kwa wateja wake.

Akizungumzia wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo Aprili 6 2022, Abel Kaseko, Mkuu Bidhaa na Mauzo kwa Wateja Binafsi, amesema kuwa kampeni hiyo itakuwa ya miezi sita na kwamba wateja wa NBC watanufaika za kampeni hiyo.

Kaseko amesema kuwa kampeni hiyo itadumu kwa muda wa miezi sita na kwamba elimu itatolewa sambamba za zawadi .

Amesema kuwa wateja 80 wa benki hiyo watashinda tiketi za kushuhudia mchezo wa watani wa Jadi Simba na Yanga utakaochezwa kwenye kiwanja cha Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akifafanua juu ya kushikiri kwenye kampeni hiyo Dorothea Mabonye Meneja wa Bidhaa kwa wateja Binafsi amesema kuwa mteja wa Benki hiyo atakayeweka kiasi cha laki tatu kwa kudunduliza kuanzia leo tarehe 6 mpaka tarehe 24 Aprili 2022 atapata nafasi ya kushinda tiketi ya kushuhudi mchezo wa huo wa watani wajadi.

Amesema kuwa wateja 50 kutoka kutoka mikoa mbalimbali nchini watazawadiwa tiketi ya kuhudhuria kwenye mtanange huo utakachezwa tarehe 30 Aprili na kwamba washindi hao watagharamiwa Chakula na malazi wakiwa jijini.

Mabonye amesema kuwa wateja 30 kutoka jijini Dar es Salaam watazawadiwa tiketi ya VIP kwenye mchezo huo.

Mbali na zawadi hiyo Mabonye ameeleza kuwa kutakuwa na tiketi za washindi watano wa safari ya kushuhudia fainali za kombe la dunia nchini Qatari Desemba mwaka .

Mabonye amesema kuwa kutakuwa na kundi la mwanzo la washindi wa safari hiyo ambao watadunduliza kwenye akaunti zao za NBC kiasi cha Shilingi Milioni 1 kuanzia leo tarehe 6 mpaka Mwezi Septamba.

“Kundi la pili litawahusu wateja wetu watakaoweka kwa kudunduliza kiasi cha shilingi milioni saba kwenye akaunti zao kuanzi leo tarehe 6 Aprili mpaka mwezi Septemba , kundi hili litakuwa linawashindi wawili watakaozawadiwa tiketi za safari ya Qatari, malazi, vyakula na vinywaji na kushuhudia mechi kwenye fainali za kombe la dunia . Hawa watapata tiketi za mzunguko”,amesema Mabonye.

Mabonye ametoa wito kwa watanzania kufungua akaunti kwenye benki hiyo ili kunufaika na kampeni hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad