HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 25, 2022

WAZIRI MAKAMBA AELEZA MAFANIKIO YA SEKTA YA NISHATI NA MIKAKATI YA KUENDELEZA SEKTA

 MKUTANO wa 15 wa Baraza la Kisekta la Kilimo na Usalama wa Chakula la Jumuiya ya Afrika Mashariki (SCAFS) leo tarehe 25 Machi 2022 umefikia tamati jijini Dar es Salaam.


Mkutano huu ambao umefanyika kwa kipindi cha siku 5 kuanzia tarehe 21 hadi 25 Machi 2022 umetimishwa katika ngazi ya Mawaziri ambapo awali, ulitangulia na Mkutano katika ngazi ya Wataalum Waandamizi uliofanyika tarehe 21 hadi 23 Machi 2022, na Makatibu Wakuu tarehe 24 Machi 2022.

Miongoni mwa masuala yaliyojitokeza katika Mkutano huo ni pamoja na kujadili ripoti za; Usalama wa Chakula na Lishe wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kupitia na kutathimini utekelezaji wa maagizo na maamuzi mbalimbali yaliyofikiwa katika Mikutano ya awali ya Baraza la Mawaziri na Baraza la Kisekta, utekelezaji wa azimio la Malabo kuhusu Progaramu ya Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika (Comprehensive Africa Agriculture Development Programme - CAADP) pamoja na uwianishaji wa pembejeo za kilimo; maendeleo ya mifugo, uvuvi na ufugaji wa samaki katika Jumuiya.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano huo wa ngazi ya Mawaziri Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayesimamia Sekta za Uzalishaji na Huduma za Jamii Bw. Christophe Bazivamo ameeleza kuwa licha ya changamoto za Janga la UVIKO-Jumuiya imerekodi mafanikio makubwa katika utekelezaji wa makubaliano na maagizo ya Baraza la Kisekta na Baraza la Mawaziri.

“Tumepiga hatua kubwa katika kuwezesha mazingira mazuri ya sekta ya kilimo kwa kuhakikisha upatikanaji na upatikanaji wa pembejeo; kuimarisha utendaji wa minyororo ya thamani ya kilimo na biashara ya bidhaa za kilimo” Amesema Bazivamo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mkutano huo na Katibu Mkuu wa Uvuvi, Kilimo na Uchumi wa Buluu wa Kenya Dkt. F.O. Owino akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Uvuvi, Kilimo na Uchumi wa Buluu wa Kenya amepongeza hatua iliyofikiwa katika utekelezaji mpango uwianishaji wa pembejeo za kilimo; maendeleo ya mifugo, uvuvi na ufugaji wa samaki katika Jumuiya.

Vilevile Dkt. Owino amepongeza dhamira za nchi Wanachama wa Jumuiya ya kuweka katika mazingira wezeshi kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya kilimo. Ameongeza kuwa uwekezaji huo utachochea ongezeko la ubora wa mazao na uzalishaji, sambamba na kuimarisha mnyororo wa thamani katika sekta ya kilimo na hatimaye kukuza biashara ya kikanda na kimataifa ya mazao ya kilimo.

Bw. Bazivamo kwa niaba ya Mkutano huo amewashukuru Washirika wote Maendeleo wakiwemo USAID Kenya na Afrika Mashariki (USAID/KEA, Idara ya Kilimo ya Marekani (USDA) na Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika lake la GIZ, Mpango wa Kuzuia na Kukabili Ugonjwa wa Mlipuko kwa msaada wao katika kuboresha sekta ya Kilimo na Usalama wa Chakula kwenye Jumuiya.

Katika Mkutano huo Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki ambaye pia aliongoza wa Ujumbe wa Tanzania, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Antony Peter Mavunde, Makatibu Wakuu, Maafisa Waandamizi wa Taasisi na Idara mbalimbali za Serikali. Aidha, Mkutano huo umehudhuriwa na nchi zote sita (6) Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.


1. Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki (Mb) ambaye pia alikuwa Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania akichangia hoja kwenye Mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Kilimo na Usalama wa Chakula la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam. Machi 25, 2022



2. Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Antony Peter Mavunde (Mb) akifuatilia Mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Kilimo na Usalama wa Chakula la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Dar es Salaam. Machi 25, 2022



3. Mkurugenzi Msaidizi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Benjamin Mwesiga (wakwanza kushoto) akifuatilia Mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Kilimo na Usalama wa Chakula la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Dar es Salaam.



4. Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki akisaini ripoti ya Mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Kilimo na Usalama wa Chakula la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam



5. Mawaziri walioshiriki Mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Kilimo na Usalama wa Chakula la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakisaini ripoti ya Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad