HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 8, 2022

WAZIRI DOROTH GWAJIMA NITAMUOMBA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUZINDUA JUKWAA KUU LA BARAZA LA WANAWAKE MKOA WA PWANI

 

Waziri wa Maendeleo ya Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Doroth Gwajima akizungumza wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya Usiku wa Mwanamke wa Pwani iliyowakutanisha wanawake wa Mkoa wa Wilaya zote za Mkoa wa Pwani kwenye Ukumbi wa Destiny uliopo maeneo ya Kwa Marias Kibaha.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge akizungumza wakat hafla ya Usiku wa Mwanamke wa Pwani iliyowakutanisha wanawake wa Mkoa wa Wilaya zote za Mkoa wa Pwani kwenye Ukumbi wa Destiny uliopo maeneo ya Kwa Marias Kibaha.

Na Khadija Kalili, Kibaha
WAZIRI wa Maendeleo ya Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Doroth Gwajima amesema kuwa kutokana na Mkoa wa Pwani kutia fora kwa kuwa na mwamko wa kuwa na majukwaa imara ya wanawake atamuomba wakati wa kuzindua rasmi aje kuzindua Kitaifa Mkoani Pwani.

Waziri Gwajima alisema hayo alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya Usiku wa Mwanamke wa Pwani iliyowakutanisha wanawake wa Mkoa wa Wilaya zote za Mkoa wa Pwani kwenye Ukumbi wa Destiny uliopo maeneo ya Kwa Marias Kibaha.

Aidha amewataka wanawake katika Mimoa mingine kuiga mfano wa mwamko ulioonyeshwa na na majukwaa ya Wanawake wa Mkoa wa Pwani kwa kujiunga na majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi huku akisisitiza kuwa wanawake wote wanapaswa kujiunga kwa kuanzia katika ngazi ya kata kwa sababu yatawasaidia kuwainua kiuchumi kuanzia chini.

Usiku huo wa Mwanamke wa Pwani ambayo uliandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa na Mkoa wa Pwanj na kusimamiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Mwanasha Tumbo kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Sara Msafiri.

"Pwani ninyi ni kinara wa agenda hii ya uanzishwaji wa majukwaa ya Wanawake huku lengo kubwa likiwa kumuwezesha mwanamke kiuchumi hivyo nawapongeza sana hasa mnavyoongelea kufungua Kiwanda chenu hili siyo jambo dogo hivyo kabla ya mwezi wa tatu haujaisha mimi nitakuja Pwani kuwatembelea Ili tuweze kujadiliana namna ya kuweza kuupaisha zaidi Mkoa wenu" alisema Dkt. Gwajima.

"Wanawake wote wa Mikoa mingine wanatakiwa wajiunge na majukwaa ya wanawake Ili waweze kupata mikopo ambayo itawawezesha kiuchumi, ila kwa wale ambao hawajajiunga na majukwaa haya wanatuchelewesha lakini hawatoweza ninachosema hapa ni kwamba wapewe hamasa zaidi Ili waweze kujiunga na majukwaa hayo Ili waweze kuvuka hapo walipo"alisema Gwajima.

Gwajima alisema kuwa mabaraza hayo ambayo kwa sasa yako katika ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa huku ngazi ya Kata yakiwa hayana nguvu sana yamefanya vizuri ambapo wanawake waneweza kujiinua kiuchumi.

"Tumpongeze Rais wetu wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan kwa wa kuyawezesha kwa kuwapatia fedha za mikopo ambapo yameleta mabadiliko makubwa kiuchumi kwa wanawake ifike wakati sasa yaanzie ngazi ya kata," alisema Gwajima.

" Pwani ya sasa siyo ya kucheza ngoma na mdundiko ya sasa imebadilika haya ndiyo mawazo tunayoyataka,"alisema Gwajima.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge alisema kuwa Rais Samia ameonyesha uwezo wa mwanamke katika ukombozi kwao hivyo anampongeza sana ambapo anatimiza mwaka mmoja tangu alipoingia madarakani mwezi Machi mwaka jana.

Kunenge alisema kuwa kwa sasa watoto wa kike wa Mkoa wa Pwani wanapata elimu na hata kama wakichezwa ngoma hawapewei mume wanapewa elimu hio ni jambo la kuwapa pongezi huku akisisitiza kuwa mila na desturi ni muhimu lakini elimu ni muhimu zaidi.

Naye mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani Farida Mgomi alisema kuwa wanawake wamenufaika sana na wanakila sababu ya kumshukuru Rais kwa kazi kubwa anayoifanya.

Mgomi alisema kuwa wao kama viongozi wa chama serikali watamuunga mkono kwa kumkwamua mwanamke kiuchumi na kuhamasisha kujiunga na majukwaa hayo ya kiuchumi ili kila mwanamke uchumi wake

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad