HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 30, 2022

WAZIRI DKT. NDUMBARO ATETA NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI, DKT. DONALD WRIGHT KUHUSU SWICA

 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro leo Machi 29 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright kuhusu masuala mbalimbali ya Uwekezaji Mahiri katika Vitalu vya Uwindaji wa Wanyamapori

Katika mazungumzo hayo Waziri Dkt.Ndumbaro amemueleza Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuweka mazingira rafiki ya Uwekezaji kwa Wawekezaji wa kutoka Marekani hususani  katika sekta ya Uwindaji wa Kitalii kwa kuzingatia maslahi ya nchi

" Moja ya shabaha yetu kama Wizara ni kuwavutia Wawekezaji, tunafanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha Wawekezaji wa kutoka nchi mbalimbali wakiwemo wa Marekani wanawekeza katika uwekezaji huu wa muda mrefu'' amesisitiza Dkt. Ndumbaro

 Wizara ya Maliasili na Utalii inatarajia kukusanya Sh23 bilioni kwa mwaka kutokana na uwekezaji mahiri unaoendekea kufanywa kwenye sekta ya utalii nchini


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia), akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright kuhusu masuala mbalimbali ya Uwekezaji Mahiri katika Vitalu vya Uwindaji wa Wanyamapori . Kikao hicho kimefanyika leo Jijini Dar es Salaam Picha na WMUWaziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia), akiagana na Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright mara baada ya kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Uwekezaji Mahiri katika Vitalu vya Uwindaji wa Wanyamapori . Kikao hicho kimefanyika leo Jijini Dar es Salaam Picha na WMU

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia), akizungumza na Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright kuhusu masuala mbalimbali ya Uwekezaji Mahiri katika Vitalu vya Uwindaji wa Wanyamapori . Kikao hicho kimefanyika leo Jijini Dar es Salaam Picha na WMU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad