HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 31, 2022

WAHAMIAJI HARAMU 74 KIZIMBANI

RAIA wa Burundi na Kongo wapatao 74, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikibaliwa na tuhuma za kuishi nchini bila kuwa na kibali.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali kutoka Uhamiaji Godfrey Ngwijo imewataja baadhi ya washtakiwa hao kuwa ni, Hasafu Amos, Justine Sefana, Herisone Jackson, Richardmaftali Lucas, David Musa na Alex Silvester.

Washtakiwa hao wamefikishwa mbele ya Mahakimu wawili tofauti ambapo, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Yusto Ruboroga inadaiwa washtakiwa 59 ambao ni Raia wa Burundi na Kongo DRC walikamatwa wakiishi nchini Tanzania bila ya kuwa na kibali au nyaraka za kuwawezesha kufanya hivyo.

Washtakiwa 15 raia wa Burundi wamesomewa shtaka lao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Avodia Kyaruzi na kudaiwa kuwa, Machi 30, 2022 katika sehemu tofauti tofauti jijini Dar es Salaam washtakiwa walikamatwa wakilishi nchini Tanzania bila ya kuwa na kibali au nyaraka za kuwawezesha kuishi nchini humo.

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Kesi hiyo itatajwa tena Aprili 6, mwaka huu.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad