UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UFARANSA, TAHA WATANGAZA BIDHAA ZA HORTCULTURAL - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 4, 2022

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UFARANSA, TAHA WATANGAZA BIDHAA ZA HORTCULTURAL

 


Na Mwandishi Wetu

UBALOZI  wa Tanzania nchini Ufaransa kwa kushirikiana na taasisi ya kuendeleza sekta ya horticulture Tanzania (TAHA), umefanya Mkutano wa kutangaza fursa za bidhaa za matunda na mbogamboga (horticultural products) za Tanzania ili kuingia kwenye soko la nchi za Ulaya hususan Ufaransa.

Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Ubalozi na kuhudhuriwa na wafanya biashara wakubwa wa sekta hiyo.  Katika mkutano huo, Mtendaji Mkuu wa (TAHA), Dkt Jacqueline Mkindi alielezea kuhusu ubora wa mazao kutoka Tanzania ambayo yanaweza kuuzwa katika soko la Ufaransa na la ulaya.

Katika taarifa yake, alisema kwamba tayari bidhaa nyingi zimeshaanza kuuzwa katika masoko mengi ya nchi za Ulaya na sasa anataka mazao hayo kuingia kwa wingi na kupata masoko nchini Ufaransa.

 TAHA ilitia saini Mkataba wa  Makubaliano (MOU) na kampuni ya Laparra ya Ufaransa, ambao ni waingizaji na wauzaji wakubwa wa mazao ya horticulture katika masoko ya Ufaransa. Makubaliano hayo yanalenga katika kutangaza na kuuza bidhaa (promotion and branding), katika masoko ya ndani na nje ya Ufaransa ikiwa ni mkakati wa kuendeleza sekta hiyo nchini Tanzania.

Kabla ya mkutano huo, Dkt Jacqueline Mkindi akiambatana na Mhe. Balozi Samwel W. Shekukindo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa walipata fursa ya kutembelea soko la kimataifa la Rungis (Soko kubwa kuliko yote la mazao ya kilimo katika bara la Ulaya).

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Samwel W. Shelukindo pamoja na Mtendaji Mkuu wa taasisi ya horticulture (TAHA), Dkt. Jacqueline Mkindi (walioketi), wakiwa katika picha ya pamoja na washirika (partners),walioshiriki katika mkutano wa kutangaza fursa za bidhaa za matunda na mbogamboga za Tanzania kuingia kwenye soko la Ufaransa 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad