HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 4, 2022

RC PWANI AZINDUA SHEREHE ZA SIKU YA WANAWAKE WILAYA YA KIBAHA

 




Na Khadija Kalili , Kibaha


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amemwagia sifa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameonyesha nafasi na uwezo wa Mwanamke duniani kutokana na uwezo wake mkubwa ameonyesha katika kuwajibika.

Amesema hayo wakati akizindua siku ya Wanawake duniani kimkoa katika viwanja vya Mailimoja mjini Kibaha na kuhudhuriwa na akinamama kutoka mkoa mzima wa Pwani.

Alisema hata wale ambao walikua na mashaka juu ya uongozi wa mwanamke kwa sasa kutokana na namna anavyoupiga mwingi hawana la kusema hivyo wanawake wote tembeeni kifua mbele kwani tunaye Kiongozi imara na madhubuti mwenye jinsia ya kike.

Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa amewataka wadau wote wanaojishughulisha na masuala ya malezi ya watoto wa kike wakajifunze kwenye shirika lisilokuwa la kiserikali la Room to read ambalo linamuhudumia mtoto wa kike katika shule za msingi na sekondari za serikali kwa kutoa mafunzo ya stadi za maisha.

Alisema jinsi shirika hilo la Room to read linavyotoa ushauri, msaada wa vifaa na ushirikishwaji wa familia shule na jamii sambamba, elimu ya fedha na ujasiriamali na masuala ya usomaji na maktaba ni mbinu madhubuti katika kukusaidia moto wa kike na mwanamke kwa ujumla kujilinda hadi afikie malengo yake.

Aidha Alhaji Kunenge amewataka wanawake wajasiriamali kujituma zaidi Ili kuweza kujikomboa kiuchumi kwa kuleta maendeleo ndani ya familia na Taifa kwa ujumla.

RC Kunenge amesema haya leo Machi mbili katika viwanja vya Maili Moja Wilayani Kibaha alipokuwa akizindua sherehe za kuelekea siku ya Wanawake Duniani ambayo itaadhimishwa duniani kote ifikapo Machi nane ambapo kwa Mkoa wa Pwani maadhimisho haya yatafanyika kimkoa katika Halmashauri ya Chalinze huku kauli mbiu ya mwaka huu inasema 'Haki na Usawa kwa maendeleo Endelevu'.

Mkuu huyo wa Mkoa amewaahidi wajasiriamali hao kuwa atakutana nao Ili waweze kujadili masuala mbalimbali yanayo wahusu na siku hiyo atajaa nao kama Alhaji Kunenge huku akisisitiza kuwa wawe huru siku hiyo katika kuzungumza nae kwa kinaga ubaga.

"Tutakaa nawenzangu tuangalie namna ya kuweza kutoa mkopo wenye tija utakaomwezesha mkopaji kufanya jambo la maana pia tutawasaidia kuwapa mafunzo na miongozo Ili wakopaji waweze kukopeshwa wakishafanikiwa waweze kukopeshwa wengine hili liko ndani ya uwezo wetu nitalijadili na Kamati yangu"alisemaKunenge.

Kila kikundi tutawafikia hakuna kundi au mtu atakayeachwa tutajitahidi tufungue fursa zaidi kwani njia ya kuwasaidia nyie ni kutoa fursa zaidi za kibiashara ,tuzingtie sheria na tutumie fursa.

"Tuhakikishe sisi sote tunashiriki katika sensa ya watu na makazi tujitokeze tushiriki vizuri na tupate chanjo za ugonjwa wa UVICO 19 takwimu zinaonyesha katika nchi yetu wale ambao hawajapata chanjo ndiyo wanaopata madhara zaidi" alisema Kunenge.

Katika sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Kamati ya Ulinzi na Usala ya Mkoa wa Pwani wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Pwani (UWT)Farida Mgomi ambaye alisema kuwa uzinduzi huu utaambatana na kufanyika maonyesho ya bidhaa mbalimbali za wajasiriamali wa Wilaya Kibaha huku akitoa wito kwa wakazi wa Wilayani hapa kujitokeza katika kuwaunga mkono.

"Alisema kuwa baada ya uzinduzi huu Machi sita kutafanyika usiku Maalumu utakaofahamika kwa jina la Usiku wa wa Mwanamke wa Pwani ambapo kutafanyika mambo mbalimbali hasa kujua Mila na desturi za Mkoa waPwani' alisema Mwenyekiti huyo.

Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Pwani Subira Mgalu ametoa pongezi kubwa kwa Wilaya na Mkoa kuandaa sherehe hizi ambazo kilele chake ni Machi nane .

Mkuu wa Wilaya Sara Msafiri alisema kuwa mwaka huu Wilaya imejipanga hivyo wataendelea kutoa misaada mbalimbali ikiwemo kwenda kutembelea waginjwa katika Hospitali ya Ocean Road, gereza la Mkuza ambapo baadhi ya wanawake kutokaWilayani hapa watakwenda kutoa misaada.

"Tumejipanga kuwajengea uwezo kina mama kwa kuwapa mafunzo Maalumu Ili waweze kupanda madaraja katika biashara zao mwisho napenda kywashukuru wadhamini wetu ambao ni NMB, TRA, OSHA,TARURA,ROOM TO READ,TANESCO,DAWASA,TAKUKURU,.

Bendi ya muziki wa dansi ya Ruvu JKT ilitumbuiza sambamba na wasanii wengine kama Msaga Sumu, Yuda wote walinogesha uzinduzi huo

Maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani ilianzishwa mwaka 1908 na kwa sasa inaadhimishwa mwaka 101.

 












No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad