HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 4, 2022

Timu ya Taifa ya Pool yaifunga Kenya 13 – 9 mashindano Afrika Nchini Zambia

Timu ya Taifa ya Pooltable ya Wanaume na Wanawaake wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mashindano ya Afrika yaliyoanza leo Lusaka Zambia kwakushirikisa Nchi saba ambazo ni Tanzania, Uganda, Kenya, Afrika Kusini, Zimbabwe, Swaziland na wenyeji Zambia.

=========  =======

TIMU ya Taifa ya Pooltable Waanaume imeanza vyema mashindano ya Afrika kwakuwafunga majirani Kenya kwa idadi ya mabao 13-9 katika mchezo wake wa kwanza wa mashindano hayo yaliyoanza leo nchini  Zambia. 

Mashindano hayo yameanza kwa makundi A na B ambapo kundi A ni Tanzania, Kenya, Uganda na Zimbabwe wakati kundi B ni Afrika Kusini, Swaziland na wenyeji Zambia. 

Jumla ya nchi saba zikiwakilishwa na timu ya Wanaume na Wanawake zinashiriki mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka. Meneja wa Timu ya Taifa , Omary Soup ametamba kufanya vizuri katika mashindano hayo kutokana na vikosi vya timu ya Wanaume na Wanawake alivyosafiri navyo kuwa imara. 

Omary alitaja wachezaji wanaowakilisha nchi kupitia mchezo wa Pool kwa upande wa Wanaume ni Abdallah Hussein, Mussa Mkweja, Baraka Jackson, Baraka Joachim, Festo Yohana, Melkzedeck Amedeus, Jackson Steven, Isaya Paul, Amos Boniphace, Innocent Sammy na Nahodha wao Charles Venance wakati timu ya Wanawake ni Neema Hamis, Grace Shitindi, Rebecca Magaigwa na Jackline Titto Mashindano yameanza leo na yanatarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki huko Lusaka Zambia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad