NBAA YAENDELEA KUTOA MAFUNZO KWA WANAFUNZI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 4, 2022

NBAA YAENDELEA KUTOA MAFUNZO KWA WANAFUNZI

Afisa Mdhibiti wa Viwango wa NBAA, CPA Winnington Makaka(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya walimu na wanafunzi wa Kidato cha Sita wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab mara baada yakumaliza ziara ya kutembelea ofisi za NBAA zilizopo jijii Dar es Salaam.

Afisa Mdhibiti wa Viwango wa NBAA, CPA Winnington Makaka akitoa elimu kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab waliotembelea na kupata mafunzo katika ofisi za Bodi ya NBAA.
Mkaguzi wa ndani wa NBAA, CPA George Lazaro akitoa elimu kuhusu kazi za wakaguzi kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab waliotembelea na kupata mafunzo katika ofisi za Bodi ya NBAA.
 
Na Mwandishi Wetu
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania (NBAA) imeendelea kutoa elimu/mafunzo kwa wanafunzi wa Taasisi, Vyuo pamoja na Shule za Sekondari ikiwa na lengo la kuwajengea ufahamu kuhusu shughuli mbalimbali za Bodi na kukuza taaluma ya Uhasibu.

Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo hayo Mdhibiti wa Viwango wa NBAA, CPA Winnington Makaka amesema si kila aliyesomea uhasibu anaweza kufanya kazi za kihasibu bali inabidi kufanya mitihani ya Bodi hiyo ili kupewa cheti cha kitaaluma ili uweze kutambulika kama Mhasibu na kuweza kufanya kazi nje na ndani ya nchi.

Aliongeza kuwa wanafunzi wa Kozi nyingine ambazo hazihusiani na masomo ya Uhasibu nao wana nafasi ya kufanya mitihani ya Bodi na wataanzia masomo ya ngazi ya kwanza (foundation level) tofauti na wale waliosomea masomo ya Uhasibu na pia waliomaliza kidato cha nne na sita na wanacheti wanaweza kufanya mitihani ya Bodi alisema Makaka.
 
Naye Mkaguzi wa ndani wa NBAA CPA George Lazaro ametoa elimu kuhusu tofauti iliyopo kati ya Mkaguzi na Mhasibu na kuainisha kazi za wakaguzi kwa wanafunzi wa Kidato cha sita wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab waliotembelea ofisi za Bodi ya NBAA Dar es Salaam ili kujifunza juu ya Taaluma hiyo.

Akiishukuru Bodi hiyo,  mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Baobab Stephen Gervas Mahundi amesema Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania (NBAA) imetoa elimu kwa wanafunzi wa kidato cha sita wa wanaosoma masomo ya biashara katika shule hiyo na elimu hiyo iliyotolewa itawasaidia wanafunzi wa Baobab katika masomo yao na kwa hapo baadae.
Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA Magreth Kageya akitoa ufafanuzi kuhusu kazi zinazofanywa na bodi hiyo wakati wa mafunzo kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab waliotembelea na kupata mafunzo katika ofisi za Bodi ya NBAA zilizopo jijini Dar es Salaam leo.
Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Baobab Stephen Gervas Mahundi akitoa neno la shukrani kwa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania (NBAA) mara baada ya wanafunzi wa Kidato cha Sita wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab mara baada ya kumaliza ziara yao walipotembelea ofisi za Bodi ya NBAA zilizopo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab wakifuatilia mada kwa wataalam kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (​NBAA) walipotembelea ofisi za Bodi hiyo zilizopo jijini Dar es Salaam leo.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad