Afisa
Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Bagamoyo Bw.Alidis Kaziyareli
ameipongeza Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa
kuendelea kuibua vipaji vya vijana wa Kitanzania kupitia sanaa
mbalimbali.
Bw.Kaziyareli alitoa pongezi hizo wakati akisoma
hotuba kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo katika Mahafali ya
wahitimu wa Mafunzo ya muda mfupi katika Chuo cha TaSUBa, ambao
wamefadhiriwa na wafadhiri mbalimbali.
Amesema kuna umuhimu wa wahitimu kuhakikisha wanazitafuta fursa kupitia mafunzo waliyoyapata na wasisubiri fursa ziwafuate.
Nae
Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt. Herbert
Makoye amesema kampuni ya TCC PLC imekuwa ikidhamini vijana kupata
mafunzo ya sanaa katika Chuo hicho tokea mwaka 2017 na vijana hao
wanahitimu wakiwa wamejengeka vyema kabisa.
“Wahitimu wanaohitimu
leo ni Vijana waliofadhiriwa na Taasisi ya TULIA TRUST vijana 25 na
wengine wamefadhiriwa na Kampuni ya MUSICIANS FOR A BETTER LIFE vijana
wapatao 58”. Amesema Dkt.Makoye.
Aidha Dkt.Makoye amewataka
wahitimu kuwa Mabalozi wazuri kwa wengine ambao watahitaji kujiunga na
Chuo hicho ili nao waweze kukuza vipaji vyao.
Kwa upande wake
mwakilishi wa Wahitimu wa mafunzo, akitoa risala mbele ya Mgeni rasmi,
Martine Mwangomale amesema kupitia mafunzo walioyapata ya muda mfupi
yamewasaidia kuongeza ujuzi na maarifa katika Sanaa ambayo wamekuwa
wakiifanya, Pia wameweza kushirikiana na kubadilishana mawazo baina yao
na Walimu waliokuwa wakiwafundisha Chuoni hapo.
Amesema muda wa
kushiriki mafunzo hayo yalikuwa ni mafupi hivyo wameomba Kwa wakati
mwingine mafunzo kama hayo yatolewa Kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja.
Pamoja
na hayo wamewashukuru walimu kwa kutoa ushirikiano wa kutosha tangu
walipofika chuoni hapo na kuanza mafunzo, kwani ushirikiano walioupata
umewajengea uelewa mkubwa kupitia mafunzo hayo.
“Tunamshukuru
mama yetu Dkt.Tulia Ackson Mwansasu Kwa kutupatia fursa hii nzuri ya
kuendeleza vipaji vyetu katika Sanaa”. Alisema Mwangomale.Afisa
Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Bagamoyo Bw.Alidis Kaziyareli
akizungumza katika mahafali ya Wahitimu wa mafuzo mafupi ya sanaa Chuoni
TaSUBa, wakati wa Mahafali yaliyofanyika chuoni hapo,Bagamoyo mkoani
Pwani
Mkuu
wa Taasisi ya Sanaa na Utamduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt. Herbert Makoye
akizungumza mbele ya Meza kuu na Wahitimu wa mafunzo ya muda mfupi
(hawapo pichani) Chuoni TaSUBa, wakati wa Mahafali yaliyofanyika chuoni
hapo,Bagamoyo mkoani Pwani
Baadhi
ya Wahitimu wa Mafunzo ya Sanaa waliofadhiriwa na Shirika la MUSICIANS
FOR A BETTER LIFE wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo
Mkurugenzi
wa shirika la MUSICIANS FOR A BETTER LIFE kutoka nchini Ujerumani Prof
Anne Buter akizungumza mbele ya Meza kuu na Wahitimu wa Mafunzo ya sanaa
ya muda Mfupi (hawapo pichani) wakati wa Mahafali yaliyofanyika mjini
Bagamoyo mkoani Pwani.
Naibu
Mkuu wa Chuo, Mipango fedha na Utawala Emmanuel Bwire akizungumza mbele
ya Meza kuu na Wahitimu wa mafunzo ya muda mfupi (hawapo pichani)
Chuoni TaSUBa, wakati wa Mahafali yaliyofanyika chuoni hapo,Bagamoyo
mkoani Pwani
Afisa
Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Bagamoyo Bw.Alidis Kaziyareli
akimkabidhi cheti kwa mmoja wa Wahitimu wa mafunzo ya Muda mfupi ya sanaa
Chuoni TaSUBa, Mahafali hayo yamefanyika mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
Mkuu
wa Taasisi ya Sanaa na Utamduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt. Herbert Makoye
akifurahia jambo na mmoja wa wahitimu wa Mafunzo ya Sanaa ya Muda mfupi
Jose George kutoka jijini Mbeya baada ya kukabidhiwa cheti chake cha
kuhitimu na Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Bagamoyo
Bw.Alidis Kaziyareli kwenye Mahafali yaliyofanyika TaSUBa mjini Bagamoyo
mkoani Pwani. Taasisi ya TULIA TRUST imewafadhiri vijana 25 kutoka jijini Mbeya kusoma TaSUBa na kihitimu mafunzo yao ya sanaa ya muda mfupi.
Meza kuu ikifuatilia burudani mbalimbali zilizokuwa zikitolewa jukwaani na Wahitimu.
Wanafunzi
Wahitimu wa mafunzo ya Sanaa ya muda mfupi wapatao 25 waliofadhiriwa na
Taasisi ya TULIA TRUST wakiwa katika picha ya pamoja na Meza kuu.
Wanafunzi
Wahitimu wa mafunzo ya Sanaa ya muda mfupi wapatao 58 waliofadhiriwa na
shirika la MUSICIANS FOR A BETTER LIFE la nchini Ujeremani wakiwa
katika picha ya pamoja na Meza kuu. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG.
No comments:
Post a Comment