HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 12, 2022

HEDHI SIO UGONJWA, JAMII YATAKIWA KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI KWA MABINTI WAWAPO KWENYE HEDHI

Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

KAMPENI ya ugawaji wa taulo za kike Kwa baadhi ya shule iliyoandaliwa na Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) lahitimishwa rasmi  katika wiki ya Kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia Mkoani Arusha.

Akizungumza na wanafunzi pamoja na walimu ,Kaimu Katibu Mkuu wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) Mkoa wa Arusha ,Asha Rashid mara baada ya kutembelea shule ya Sekondari Arusha girls amesema ni muhimu jamii inayomzunguka mtoto wakike iwe chachu na silaha ya kumjengea uwezo na Mazingira rafiki  Binti na kujiona wa fahari pale anapokuwa kwenye Hedhi Ili aweze kujiamini.

"Hedhi sio ugonjwa Wala sio kitendo Cha aibu hivyo ni muhimu jamii ikatambua kuwa wanayohaki ya kuhakikisha binti huyo anajikubali na kuendelea na Majukumu yake ya kimasomo Huku ikimuhakikishia anapata taulo Kwa mlengo wa kujihifadhi kabidhi taulo za Kike awapo  shuleni."

Aidha,kaimu huyo ameeleza lengo la kuchagua shule ya Sekondari ya Arusha girl amesema ni Kutokana na kuwepo uhitaji wa taulo hizo hususani Mabinti wanapokua shuleni Shirika hilo limewiwa kutoa zawadi hizo Kwa wanafunzi hao.

Hata hivyo mbali na kutoa zawadi hizo Shirika hilo lilitoa  Elimu kwa Mabinti hao kuhusu Hedhi Salama pamoja na kuvunja upendeleo Ili kuleta Mabadiliko (Bias) katika Taifa letu na kuhakikisha Kila Binti anafikia Malengo.

Kaimu Katibu wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) Tawi la Arusha Asha Rashid akimkabidhi Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Arusha girls box la taulo za kike mara baada ya kumaliza Kampeni ya uongozi wa Shirika hilo kutembelea baadhi ya shule za Sekondari nchini kugawa taulo kama sehemu ya Kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia.
Picha ya pamoja ya uongozi wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) wakiwa na Katibu wa Shirika hilo Asha Rashid wakiwa katika shule  ya Sekondari Arusha girls mara baada ya kukabidhi taulo za kike wakisikiliza machache kutoka Kwa wenyeji wao

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad