HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 19, 2022

Benki ya NBC yaahidi ushirikiano zaidi Zanzibar

 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Baraza la Wakillishi wa Zanzibar waliotembelea ofisini kwake leo.

 =======   ========    =======

Benki ya NBC imeahidi kutanua wigo wa mtandao wake wa huduma ili kuwafikia wanachi wengi zaidi visiwani Zanzibar. Akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliotembelea ofisini kwake Dsm  leo, Mkurugenzi Mtendaji Benki ya NBC, Theobald Sabi amesema kuwa Benki hiyo iko mbio kufungua milango zaidi visiwani humo ili kuendana na kasi ya ujenzi wa uchumi wa Bluu.

 
“Benki ya NBC ikiwa ni mdau mkubwa wa maendeleo nchini, imedhamiria kuongeza njia za kutolea huduma Zanzibar ili kuwafikia wananchi wengi zaidi. Pamoja kuongeza  mtandao wa matawi,  pia tutaongeza wigo wa Mawakala wetu na kuwekeza zaidi katika huduma za kidijitali na kushiriki zaidi katika miradi ya maendelo ili kuchochea zaidi ukuaji wa uchumi” alisema Sabi.
 
Kwa upande wake, mkuu wa msafara huo, Mh. Miraji Khamis, Muwakilishi wa Chumbini Zanzibar, aliishukuru Benki ya NBC kwa kuendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo ya kiuchumi ya Zanzibar na kuahidi kutoa ushirikiano zaidi kwa faida ya pande zote mbili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad