HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 24, 2022

ZINAHITAJIKA ZITIHADA ZA KUDHIBITI UKATAJI MITI HOLELA - MAGANGA

 

 

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga amesema zinahitajika hatua za haraka katika kudhibiti vitendo vya ukakaji miti kiholela pamoja na uharibifu wa misitu.

Pia amesema uharibifu wa misitu unachangiwa kwa kiasi kikubwa na shughuli zisizo endelevu za binadamu pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi akitahadharisha ikiwa hali hii haitadhibitiwa, takriban miaka 40 hadi 50 kutoka sasa, nchi yetu itakuwa katika hatari ya kugeuka kuwa jangwa.

Bi. Maganga amesema hayo wakati akizindua Mradi wa Kujenga Uwezo wa Taasisi ili kupunguza Hewa ya Ukaa inayosababishwa na Ukataji wa Miti na Uharibifu wa Misitu (REDD+) leo Februari 23, 2022 mjini Morogoro.

Bi. Maganga alibainisha kuwa ukataji miti na uharibifu wa misitu huchangia mabadiliko ya tabianchi ambao husababisha uzalishaji wa hewa ya ukaa kwa asilimia takriban 20 duniani.

Alisema kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa unaotokana na ukataji wa miti na uharibifu wa misitu ni makubaliano ya kimataifa yanayosisitiza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia kupunguza utoaji wa gesi joto.

Katibu mkuu aliongeza kuwa Tanzania Bara inakadiriwa kuwa na jumla ya hekta milioni 48.1 za misitu ambayo ni takriban asilimia 55 ya eneo lote na takriban hekta 106,458 za misitu Tanzania Zanzibar ambayo ni takriban asilimia 41 huku akibainisha ukataji miti kwa mwaka wa Tanzania Bara unakadiriwa kufikia hekta 469,420 ambapo kwa Zanzibar ni 3,149.

“Misitu ina faida kubwa katika maisha ya mwanadamu na viumbe wengine, ikiharibiwa husababisha upotevu mkubwa wa bayoanuai na hatari ya kutoweka kwa baadhi ya spishi muhimu za mimea na wanyama. Kuharibika kwa bayonuai kunakadiriwa kuigharimu Serikali wastani wa asilimia 5 ya Pato la taifa kwa mwaka na kunufaisha zaidi jamii za vijijini zinazotegemea mazingira na maliasili kwa maisha yao ya kila siku,” alisisitiza.

Misitu hii ni makazi ya viumbe hai na baadhi yake ni vyanzo vya maji vinavyosaidia ustawi wa maisha yetu na maendeleo ya shughuli mbalimbali za kiuchumi nchini.

Alisema kuna haja ya kuendeleza uhamasishaji wa jamii kushiriki katika mipango ya kupunguza hewa ya ukaa kwa kupanda na uhifadhi wa misitu ambayo inanyonya hewa hiyo.

Kwa upande wake Bw. Bjern Midthun kutoka Ubalizi wa Norway alionesha matumaini yake katika mradi huo na kusema kuwa utasaidia kupunguza changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.

Alipongeza Tanzania kwa kushiriki katika mikutano mbalimbali ya kimataifa kuhusu masuala ya mazingira ukiwemo wa COP26 uliofanyika mwaka jana na kusema ni hatua nzuri katika kuhakikisha athari za mabadiliko ya tabianchi zinaondoshwa.

Nae Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba alisema kasi ya ukataji miti ni mkubwa katika nchi yetu hivyo mradi huu utasaidia kutafuta nishati mbadala ili kupunguza ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa.

Dkt. Komba alisema pia kilimo kisicho enxelevu kinachangia changamoto hizo hivyo kupitia REDD+ itatafutwa njia bora ya kufanya kilimo bila kufyeka eneo kubwa kwa ajili ya kulima badala yake kutumia eneo dogo kufanya kilimo chenye tija.

“Kupitia mradi huu wa REDD+ tunasema tuko tayari kujenga uwezo wetu hususan katika sekta ya mifugo kuhakikisha inapata sehemu nzuri ya malisho bila kuharibu vyanzo vya maji,” alisema Dkt. Komba.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akimkabidhi kitabu cha Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 iliyozinduliwa hivi karibuni na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, mara baada ya Katibu Mkuu kuzindua Mradi wa Kujenga Uwezo wa Taasisi ili kupung    uza Hewa ya Ukaa inayosababishwa na Ukataji wa Miti na Uharibifu wa Misitu (REDD+) kwa ushirikano na Serikali ya Norway leo Februari 23, 2022 mjini Morogoro.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na washiriki katika mkutano wa uzinduzi wa Mradi wa Kujenga Uwezo wa Taasisi ili kupunguza Hewa ya Ukaa inayosababishwa na Ukataji wa Miti na Uharibifu wa Misitu (REDD+) kwa ushirikano na Serikali ya Norway leo Februari 23, 2022 mjini Morogoro.
Viongozi mbalimbali wakiwa katika meza kuu wakati wa mkutano wa uzinduzi wa Mradi wa Kujenga Uwezo wa Taasisi ili kupung         uza Hewa ya Ukaa inayosababishwa na Ukataji wa Miti na Uharibifu wa Misitu (REDD+) kwa ushirikano na Serikali ya Norway leo Februari 23, 2022 mjini Morogoro.
Afisa Mazingira Mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Manyika akitoa mada wakati wa mkutano wa uzinduzi wa Mradi wa Kujenga Uwezo wa Taasisi ili kupunguza Hewa ya Ukaa inayosababishwa na Ukataji wa Miti na Uharibifu wa Misitu (REDD+) kwa ushirikano na Serikali ya Norway leo Februari 23, 2022 mjini Morogoro.

Washiriki wakiwa katika mkutano wa uzinduzi wa Mradi wa Kujenga Uwezo wa Taasisi ili kupunguza Hewa ya Ukaa inayosababishwa na Ukataji wa Miti na Uharibifu wa Misitu (REDD+) kwa ushirikano na Serikali ya Norway leo Februari 23, 2022 mjini Morogoro.
Mshauri katika Ubalozi wa Norway, Bw. Bjern Midthun akitoa neno wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kujenga Uwezo wa Taasisi ili kupunuza Hewa ya Ukaa inayosababishwa na Ukataji wa Miti na Uharibifu wa Misitu (REDD+) leo Februari 23, 2022 mjini Morogoro.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akizindua Mradi wa Kujenga Uwezo wa Taasisi ili kupung          uza Hewa ya Ukaa inayosababishwa na Ukataji wa Miti na Uharibifu wa Misitu (REDD+) kwa ushirikano na Serikali ya Norway leo Februari 23, 2022 mjini Morogoro.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad