HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 1, 2022

Yanga yawafanyia vipimo wachezaji wawili kabla ya kuwapatia leseni ya kujiunga

 

Fundi sanifu wa moyo (Cardiovascular technologist) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Paschal Kondi akimpima kipimo cha kuangalia jinsi mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography – ECG) mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Yanga Aboutwaleeb Mshery wakati wachezaji wawili wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya ya moyo kabla ya kupata leseni ya kujiunga na timu hiyo.
Radiografa wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Indrisa Juma akimpima X-ray ya kifua ili kuchunguza moyo na mapafu mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Yanga Salum Salum (Sureboy) wakati wachezaji wawili wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya ya moyo kabla ya kupata leseni ya kujiunga na timu hiyo.
Mtaalam wa maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jordan Megabe akimtoa damu mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Yanga Aboutwaleeb Mshery wakati wachezaji wawili wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya ya moyo kabla ya kupata leseni ya kujiunga na timu hiyo.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dickson Minja akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph - ECHO) mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Yanga Salum Salum (Sureboy) wakati wachezaji wawili wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya ya moyo kabla ya kupata leseni ya kujiunga na timu hiyo.

Picha na: JKCI

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad