Meneja
wa Benki ya NMB Tawi la Bagamoyoi, Bertha Mungure (katikati)
akizungumza wakati wa kuchezesha Droo ya fainali ya Bonge la Mpango II
ambapo Pikipiki 22 za miguu mitatu ziliweza kupata washindi pamoja na
pesa. kushoto ni Afisa Mkaguzi Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Pendo
Mfuru na kulia ni Afisa Huduma kwa wateja Benki ya NMB, Neema Kazoviyo.

Afisa
Huduma kwa Wateja Benki ya NMB, Neema Kazoviyo akizungumza na mmoja
kati ya washindi 22 waliojishindia Pikipiki ya Magurudumu matatu wakati
wa kuchezesha Droo ya fainali ya Bonge la Mpango II. Katikati ni Meneja
wa Benki ya NMB, Tawi la Bagamoyo, Bertha Mungure na kushoto ni Afisa
Mkaguzi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Pendo Mfuru.
…………………………………………………………………….
Kampeni
ya Benki ya NMB ya kuwahamasisha wateja wake kuweka akiba ya Bonge la
Mpango II ilifungwa rasmi wiki iliyopita kwa washindi 32 kujinyakulia
zawadi zenye thamani ya TZS milioni 100.
Miongoni
mwa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni hiyo kabambe walikuwa ni
wateja 22 wa NMB walioshinda pikipiki za miguu mitatu aina ya Skymark
ambazo bei ya kila moja ni TZS Milioni 4.5.
Pia
katika kuhitimisha shindano hilo la wiki 12 lililoanza mwezi Oktoba
mwaka jana washindi 10 walishinda TZS 100,000 kila mmoja. Lengo la
“Bonge la Mpango II” ilikuwa kurejesha fadhila kwa wateja waaminifu na
kuwahamasisha kujenga utamaduni wa kuweka akiba, na promosheni hii
imenufaisha wateja zaidi ya 170.
Kwenye
droo ya mwisho iliyofanyika katika Tawi la NMB Bagamoyo mbele ya Afisa
wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bi Pendo Mfuru, washindi 17
walitwaa pikipiki za fainali, watatu wakijibebea pikipiki za mwisho wa
mwezi na wawili walishinda pikipiki za droo ya wiki.
Hii
imekuwa promosheni yenye mafaniko makubwa sana, kwani kila wiki
washindi 10 walijishindia pesa taslimu na wawili pikipiki za Skymark,
huku droo za mwisho wa mwezi zikiwazawadia washindi watatu pikipiki hizo
za kisasa. Jumla ya Skymark 50 zilinyakuliwa kwenye kampeni hii
iliyokuwa na zawadi zenye thamani ya zaidi ya TZS. Milioni 246 ambazo
washindi wake walitoka sehemu mbalimbali nchini.
Washindi
walioshinda pikipiki za droo ya mwezi Desemba na matawi yao kwenye
mabano ni: Emmanuel Kavishe (Zanzibar), Mbila Salum (Mafinga) na Albert
Mhehe (Mkwawa).
Waliojinyakulia
pikipiki 17 za droo ya fainali ni: Frank Mgeni (Ngaramtoni), Bundala
Gwanona (Geita), Mary Martine (Kenyatta Road), Misoji Joseph (Kenyatta
Road), Martha Makorere (Tarime), Ambakisye Kyomo(Kaitaba), Paschal
Kaloli (Geita) na Herieth Alphonce (Babati).
Wengine
ni Elineema Ezekiel (Babati), Khamis Abbas (Sikonge), Hamalos Kahindi
(Nzega), Mathias Lusendamila (Manonga), Clement William (Wami), Michael
Kabume (Mvomero), Glory Mwalongo (Mvomero), Marc Constantine (Wami) na
Aziza Nzoto (Mvomero).
No comments:
Post a Comment