HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 14, 2022

TARURA KUENDELEA KUIMARISHA MTANDAO WA BARABARA UBUNGO

 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya rasimu ya bajeti kwa ajili ya miundombinu ya barabara ambapo ameitaka TARURA kuendelea kutekeleza miradi hiyo ndani ya Wilaya ili kumaliza kabisa changamoto za ubovu wa barabara.Leo jijini Dar ees Salaam.
WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA,) imewasilisha rasimu ya bajeti ya matengenezo ya barabara kwa baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 rasimu yenye bajeti ya thamani ya shilingi bilioni 3.2 fedha ambazo zimeelekezwa katika uboreshaji wa mtandao wa barabara kwa Wilaya hiyo ambao umefikia Kilomita 574.56.

Akizungumza wakati wa uwasilishwaji wa rasimu hiyo Meneja wa TARURA Wilaya ya Ubungo Mussa Mzimbiri amesema kuwa bajeti hiyo itajikita katika matengenezo ya barabara kwa maeneo korofi, maeneo maalum, vivuko pamoja na matengenezo ya kawaida kwa barabara katika Wilaya hiyo.

Mzimbiri amesema, uboreshaji wa mtandao huo wa barabara unalenga kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi na utazingatia vipaumbele vya kuhakikisha kila Kata inafikiwa na miundombinu ya barabara pamoja na kutengeneza muunganiko wa usafiri wa barabara kati ya mitaa na Kata.

Ameeeleza kuwa, uwasilishwaji wa bajeti hiyo kwa baraza na Madiwani ni katika kushirikiana katika utekelezaji miradi hiyo pamoja kuwaonesha hali halisi ya kipi kilichopo na uhitaji ili waweze kuongeza bajeti kupitia vikao vyao vya bajeti.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James ameipongeza wakala hiyo kwa kuendelea kutekeleza miradi ya barabara kwa kuhakikisha zinapitika licha ya baadhi ya barabara kuwa na changamoto.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wameipongeza TARURA kwa utendaji kazi wao na kushauri mpango huo utekeleze kwa asilimia 100 ili kumaliza changamoto ya kero za ubovu wa barabara na kuchochea shughuli za kijamii zaidi.

Mtandao wa barabara katika Wilaya ya Ubungo asilimia 91.67 ni tabaka la udongo na kiasi kidogo cha changarawe na barabara zilizo na tabaka la zege na lami ni kilomita 47.84 sawa na asilimia 8.33.


Meneja wa TARURA Wilaya ya Ubungo Mussa Mzimbiri akizungumza wakati wa uwasilishwaji wa rasimu hiyo ya bajeti na kueleza kuwa kuwa bajeti hiyo itajikita katika matengenezo ya barabara kwa maeneo korofi, maeneo maalum, vivuko pamoja na matengenezo ya kawaida kwa barabara katika Wilaya hiyo.
Matukio mbalimbali wakati wa kikao hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad