HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 20, 2022

RAIS WA ZANZIBAR AMESHUHUDIA UTIAJI WA SAINI UJENZI WA BANDARI MPYA YALIMNDI ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akishuhudia utiaji wa saini wa mpango mkuu na kufanya utafiti upembezi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa Bandari Mpya ya Malindi Zanzibar, kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar amesaini Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar.Bw.Amour Hamil Bakar, na kwa upande wa Mamlaka ya Uwekezaji ya Oman amesaini.Sheikh.Nasser Al Harthy.hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akishuhudia utiaji wa saini mpango mkuu na kufanya utafiti na upembezi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa Bandari Mpya ya Malindi Zanzibar, kwa upande wa Serikali ya Zanzibar amesaini Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Bw. Nahaat Mahfoudh na kwa upande wa Mamlaka ya Uwekezaji ya Oman amesaini Bw.Mohamed Al Tooq,hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
KATIBU Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar.Mhe Rahma Kassim Ali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza baada ya kumalizika kwa wa utiaji wa saini ya Ujenzi wa Bandari Mpya ya Malindi Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 20-1-2022.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza baada ya utiaji wa saini wa mpango mkuu na utafiti na uembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi mpya wa bandari ya malindi Zanzibar, Mamlaka ya Uwekezaji ya Oman, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Sheikh.Nasser Al Harthy (kulia kwa Rais) Balozi Mdogo wa Oman Anayefanyika Kazi zake Zanzibar Mhe Balozi.Said Salim Al Sinawi, baada ya kumalizika kwa Hafla ya utiaji wa Saini ya Ujenzi wa Bandari ya Malindi Zanzibar iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Picha na Ikulu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad