Njombe:Jumuiya ya wazazi wapanda miche 226 ya Parachichi kuadhimisha miaka 45 ya CCM - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 27, 2022

Njombe:Jumuiya ya wazazi wapanda miche 226 ya Parachichi kuadhimisha miaka 45 ya CCM

 Na Amiri Kilagalila,Njombe

JUMUIYA ya wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya na mkoa wa Njombe wameshiriki upandaji wa miche ya Parachichi 226 katika kata ya Ramadhani,ikiwa ni kuendelea kuhamasisha upandaji wa miti ili kutunza mazingira katika kuelekea kuadhimisha kutimiza miaka 45 ya kuzaliwa kwa chama hicho.

Akizungumza akiwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole amesema Chama cha Mapinduzi kinajivunia kufanikiwa katika nafasi mbalimbali za kiuchumi na kisiasa ambapo amempongeza rasi kwa kuisimamia Nchi kwa umakini.

“Tunakwenda kupanda karibu miche mia mbili ni lazima tupande kwa uangalifu ili imee vizuri na kukipata tunachokitarajia hapo baadaye na kutimiza adhma ya jumuiya zetu kuzidi kujitegemea kiuchumi”alisema Erasto Ngole

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wa CCM Mkoa wa Njombe Gerad Mpogolo na mwenyekiti wa Jumuiya Wilaya Kasanga Makweta wamesema jumuiya zihamasishe jamii kujikita katika uzarishaji mali kuinua uchumi wao pamoja na kutumia nafasi zao kuhimiza wanachama kujisajili kwenye mfumo wa usajili Kidigitali.

“Upandaji wa miti jumuiya ya wazazi ni sehemu yetu katika kipengele cha mazingira,sisi kazi yetu ni kuhamasisha na kuelimisha ili watu wapande miti na sisi leo tunaazimisha miaka hii 45 ya kuzaliwa kwa Chama chetu kwa kupanda miche ya parachichi”alisema Gerad Mpogolo

Katibu wa CCM wilaya ya Njombe Sure Mwasangute ametaka wanachama kujiandaa na uchaguzi unaofuata huku katibu wa jumuiya ya wazazi wilaya bwana EmmanueL Ngulugulu akizikumbusha jumuiya mbalimbali kuanzisha miradi ya maendeleo kwa manufaa yao.

Awali taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi iliyosomwa na diwani wa kata ya Ramadhani Bwana Nickson Nganyange imebainisha miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika kata hiyo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa katika mitaa mbalimbali.

Maadhimisho ya kutimiza miaka 45 ya kuzaliwa kwa chama hicho jana yamefanyika Mtaa wa Itulike kata ya Ramadhani ambapo kilele chake kitakuwa mwezi february 5 mwaka huu.
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wa CCM Mkoa wa Njombe Gerad Mpogolo akipanda mche wa Parachichi katika shamba lilopo katika mtaa wa Itulike Amani.
:Katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole akitoa maelekezo kwa wajumbe wa jumuiya ya wazazi namna ya kupanda mche wa Parachichi.
Baadhi ya wajumbe wa jumuiya ya wazazi wakiendelea na zoezi la kupanda miche ya Parachichi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad