NAIBU WAZIRI KASEKENYA AZINDUA MRADI WA UIMARISHAJI NA UDHIBITI WA USAFIRI WA ANGA NCHINI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 14, 2022

NAIBU WAZIRI KASEKENYA AZINDUA MRADI WA UIMARISHAJI NA UDHIBITI WA USAFIRI WA ANGA NCHINI

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi - Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amezindua mradi wa uimarishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga nchini tarehe Januari 14, 2022 uliofanyika Makao Makuu ya Usafiri wa Anga Tanzania jijini Dar es salaam.
 
Akizungumza katika hafla maalum ya uzinduzi wa mradi huo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Ujenzi - Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema fedha hizo zitatumika kuboresha miundombinu ambayo kwa sasa yanakwenda sambamba na maboresho yanayofanywa na Serikali katika Shirika la Ndege Nchini. 

“Nawapongeza sana Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), kwa kazi nzuri ambayo mmeifanya mpaka kuwa miongoni mwa Nchi chache ambazo zimepata fedha hizo, ni imani yangu kuwa hatutarudi nyuma hasa ukizingatia Serikali inaboresha Shirika letu la Ndege” amesisitiza Naibu Waziri Kasekenya. 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Bw. Johari Hamza amesema mradi huo kazi yake kubwa itakuwa ni kuhimarisha Usalama wa Usafiri wa Anga ili kuweza kupunguza au kumaliza kabisa ajali mbalimbali pia na uwepo wa watalaamu wa Usafiri wa Anga watakaopata mafunzo mbalimbali ndani ya mwaka mmoja pamoja na  upatikanaji mzuri wa vifaa bora katika kazi za usalama wa usafiri wa Anga.

Mradi huo umehudhuriwa na watu mbalimbali mwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania Xu Chen, Naibu Katibu Mkuu  wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi- Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Ali Possi, Mwakilishi wa Katibu wa ICAO Barry Kashambo, Wakurugenzi  wakuu wa Taasisi pamoja na wadau mbalimbali wa Sekta ya Usafiri wa Anga Tanzania
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi - Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akizungumza  kuhusu namna Serikali walivyojipanga kusimamia Usafiri wa Anga hapa nchini wakati wa uzinduzi wa mradi wa uimalishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga nchini uliofanyika tarehe Januari 14, 2022  Makao Makuu ya Usafiri wa Anga Tanzania, Ukonga-Banana jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S. Johari akizungumza kuhusu namna Mamlaka hiyo ilivyojipanga kutekeleza mradi wa uimalishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga wakati wa uzinduzi wa mradi wa uimalishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga nchini uliofanyika tarehe Januari 14, 2022  Makao Makuu ya Usafiri wa Anga Tanzania, Ukonga-Banana jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu  wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi- Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Ali Possi akitoa neno kwenye uzinduzi wa mradi wa uimalishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga nchini uliofanyika tarehe Januari 14, 2022  Makao Makuu ya Usafiri wa Anga Tanzania, Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la Anga Duniani, Kanda ya mashariki na kati  (Eastern and Southern African),  Barry Kashambo akizungumza kuhusu namna Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) walivyofanya kazi kwa bidii na kuitoa Mamlaka hiyo katika asilimia 30 na kufikia asilimia 67 na kufanya kupata mkopo  kutoka katika Shirika hilo uzinduzi wa mradi wa uimalishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga nchini uliofanyika tarehe Januari 14, 2022  Makao Makuu ya Usafiri wa Anga Tanzania, Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Balozi wa China, Xu Chen akizungumza kuhusu Serikali ya  Jamhuri ya Watu wa China inavyoendelea kutoa misaada kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania wakati wa uzinduzi wa mradi wa uimalishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga nchini uliofanyika tarehe Januari 14, 2022  Makao Makuu ya Usafiri wa Anga Tanzania, Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) pamoja na wadau mbalimbali wa Usafiri wa Anga wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi - Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya alipokuwa anazindua mradi wa Uimalishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga nchini uliofanyika tarehe Januari 14, 2022  Makao Makuu ya Usafiri wa Anga Tanzania, Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi - Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya  akiwa kwenye picha za pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) pamoja na wadau mbalimbali wa Usafiri wa Anga mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa mradi wa Uimalishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga nchini uliofanyika tarehe Januari 14, 2022  Makao Makuu ya Usafiri wa Anga Tanzania, Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad