MIRADI YA KIMKAKATI KUMALIZA TATIZO LA MAJI IFIKAPO 2025 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 4, 2022

MIRADI YA KIMKAKATI KUMALIZA TATIZO LA MAJI IFIKAPO 2025

 

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inatekeleza kampeni itwayo "Tunawafika wote ifikapo mwaka 2025" kwa kutekeleza miradi ya kimkakati ukiwemo mradi wa uboreshaji huduma ya majisafi kuanzia Makongo hadi Bagamoyo mkoani Pwani.

Akizungumza wakati wa kukagua utekelezaji wa mradi huo Mhandisi mshauri wa Mradi wa Makongo hadi Bagamoyo Mhandisi Jerimy Becket amesema mradi huo umehusisha ujenzi wa kituo cha kusukuma maji katika eneo la Mapinga yatakayopelekwa katika tenki la kuhifadhi maji Vikawe lenye ukubwa wa ujazo wa lita milioni 5 za maji ambapo litaenda kuwaondolea changamoto ya upatikanaji wa maji katika maeneo hayo hivyo wananchi wawape muda DAWASA ili waweze kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.

Amesema DAWASA wameanza kampeni ya kuwafikia Wateja wake ifikapo mwaka 2025 hivyo wataendelea na usimamizi wa miradi huo ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Naye mkazi wa Kinondo Adelina Elisha amesema anaishukuru Serikali ya awamu ya sita pamoja na DAWASA kwa kuweza kuwafikishi mradi wa maji katika makazi yao kwani hapo mwanzo walikuwa wanapata tabu hasa kwenye upatikanaji wa majisafi hivyo maji hayo yataziweka ndoa zao sehemu salama
Mhandisi Mkazi wa Mradi wa Chuo kikuu mpaka Bagamoyo Jerimy Becket akitoa maelezo kuhusu Pampu ya kusukumia maji ya Mapunga itakayokuwa inapeleka maji katika tenki la Vikawe lenye ujazo wa Milioni 5 za maji ikiwa DAWASA wakifanya kampeini ya kuwafia Wateja wake ifikapo mwaka 2025
Zoezi la kutoa udongo kwa ajili ya ujenzi Pampu ya kusukumia maji ya  Mapinga itakayokuwa itayopeleka maji katika tenki la Vikawe lenye ujazo wa Milioni 5 za maji ukiendelea.
Mkakuza usalama wa kazi kwenye mradi wa Maji wa Chuo Kikuu mpaka Bagamoyo, Calorine Fransis akizungumza kuhusu namna wananchi wa Kinondo watakavyonufaika na mradi wa maji ambapo wananchi zaidi ya 1000 watapata huduma ya Majisafi na salama ikiwa ni kampeini ya DAWASA ya kuwafikia wananchi wote ifikapo mwaka 2025.
Zoezi la kuchimba kwa ajili ya kulaza Bomba ili wananchi wa eneo la Kinondo likiendelea ambapo wananchi zaidi ya 1000 watafikiwa na huduma ya Majisafi na salama ambapo wananchi 750 wameishalaziwa mabomba ya maji.
Mwananchi wa Kinondo Adelina Elisha akitoa shukrani kwa DAWASA pamoja na Serikali ya awamu ya sita kwa kuweza kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji katika eneo hilo wakati wa kulaza bomba katika mtaa wa Kinondo kata ya Mabwepande
Muonekano wa mambomba ya DAWASA yaliyowafikia wananchi mbalimbali wa Kinondo.
Mwananchi wa mtaa wa Kinondo, Mwangusa akizungumza kuhusu namna walivyoupokea mradi wa maji wa Chuo Kikuu mpaka Bagamoyo unaotekelezwa na DAWASA na namna utakavyoboresha maisha hasa kwenye familia.
Ulazaji wa bomba za inchi 12 ukiendelea katika eneo la Madale
Mhandisi wa Mradi wa Chuo Kikuu mpaka Bagamoyo kutoka DAWASA, Theodore Mrosso akitoa maelezo kuhusu Bomba linaloingiza na linalotoa maji kwenye tenki la maji la Tegeta A ikiwa ni kampeini ya DAWASA ya kuwafikia Wateja wake ifikapo mwaka 2025
Mhandisi wa Mradi wa Chuo Kikuu mpaka Bagamoyo kutoka DAWASA, Theodore Mrosso akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa tenki la maji la Tegeta A litakolokuwa na ujazo wa Lita Milioni 5 pamoja na gharama zilizotumika kwenye ujenzi huo ikiwa ni kampeini ya DAWASA ya kuwafikia Wateja wake ifikapo mwaka 2025
Muonekano wa tanko la Tegeta A lenye ujazo wa Lita Milioni 5

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad