MAKAMBA AKUTANA NA MENEJIMENTI YA WIZARA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 11, 2022

MAKAMBA AKUTANA NA MENEJIMENTI YA WIZARA

Waziri wa Nishati, January Makamba (kushoto) akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba( kulia) mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara ya Nishati Jijini Dodoma tarehe 10 Januari 2022, katikati Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato.Waziri wa Nishati, January Makamba akiongoza kikao cha Menejimenti ya Wizara ya Nishati kilichofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati Jijini Dodoma tarehe 10 Januari 2022.

Waziri wa Nishati, January Makamba, akizungumza katika kikao cha Menejimenti ya Wizara ya Nishati kilichofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati Jijini Dodoma tarehe 10 Januari 2022.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, akizungumza katika kikao cha Menejimenti ya Wizara ya Nishati kilichofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati Jijini Dodoma tarehe 10 Januari 2022.Waziri wa Nishati, January Makamba (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato,( katikati) Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba(kulia) pamoja na Naibu katibu Mkuu wa Waizara ya Nishati, Kheri Mahimbali( hayupo pichani) kabla ya kuanza kikao cha Menejimenti ya Wizara kilichofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati Jijini Dodoma tarehe 10 Januari 2022.

Hafsa Omar- Dodoma
WAZIRI wa Nishati, January Makamba amekutana na menejimenti ya Wizara ya Nishati, kikao kilifanyika tarehe 10 januari, 2022 katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtumba jijini Dodoma.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati Wakili Stephen Byabato, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Naibu Katibu Mkuu, Kheri Mahimbali pamoja na viongozi mbalimbali wa Wizara hiyo na Taasisi zilizopo chini ya Wizara.

Kikao hicho cha Menejimenti kilifanyika mara baada ya mapokezi ya katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba.

Akizungumza katika kikao hicho, Makamba alimpongeza katibu mkuu wa Wizara hiyo kwa uteuzi wake alioupata hivi karibuni na kumtaka kufanya kazi kwa weledi na uadilifu.

Pia, aliwataka viongozi wa Wizara pamoja na wa Taasisi kusimamia miradi yote ya Nishati ili ikamilike kwa wakati na watanzania wafaidike na miradi hiyo.

Vilevile, aliwataka watumishi wa Wizara na Taasisi zake kufanya kazi kwa bidii na waledi ili kuleta matokeo chanya yenye tija ambayo yataleta mabadiliko nchini.

Naye, Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato alitoa pongezi zake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo na kumtakia majukumu mema.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amewashukuru Watumishi wote wa Wizara hiyo kwa mapokezi waliyomuandalia wakati alipowasili kwenye Wizara hiyo.

Aidha, ameahidi kutoa ushirikiano kwa watumishi wa Wizara hiyo na kuwataka kuumunga mkono katika majukumu yake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad