1.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akitoa
maelekezo ya kuendeleza utendaji bora kwa Taasisi za Bodi ya Filamu,
BASATA na COSOTA wakati alipofanya ziara katika Taasisi hizo katika
majengo ya Utumishi, Kivukoni jijini Dar es Salaam. Akifuatiwa na Katibu
Mkuu wa Wizara Dkt. Hassan Abbas, Naibu Katibu Mkuu Mhe. Said Othman
Yakubu na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho
Kilonzo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbas
akielezea kuhusu umuhimu wa Haki za Wasanii wakati Waziri wa Wizara hiyo
Mhe. Mohamed Mchengerwa alipozitembelea Taasisi za Bodi ya Filamu,
BASATA na COSOTA zilizopo katika majengo ya Utumishi, Kivukoni jijini
Dar es Salaam.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo akielezea
majukumu na utendaji wa Bodi hiyo wakati Waziri wa Wizara hiyo Mhe.
Mohamed Mchengerwa alipozitembelea Taasisi za Bodi ya Filamu, BASATA na
COSOTA zilizopo katika majengo ya Utumishi, Kivukoni jijini Dar es
Salaam.
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ameitaka Bodi ya
Filamu Tanzania (TFB) kuendelea kuwajengea uwezo Wadau mbalimbali wa
Tasnia ya Filamu kwa lengo la kuhakikisha Wadau hao wanakuwa na uwezo wa
kutoa kazi zenye viwango bora.
Mhe.
Mchengerwa ameyasema hayo wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea
na kujifunza majukumu ya Taasisi zilizopo katika Wizara hiyo ikiwemo
Bodi ya Filamu Jumatatu Januari 17, 2022 Jijini Dar es salaam.
Akizungumza
na Watendaji wa Bodi ya Filamu Waziri ameitaka Bodi hiyo kuendelea
kutoa elimu na kuwajengea uwezo Wadau wa Filamu ili waweze kutoa Filamu
za Kitanzania zenye ubora mzuri na uhalisia zitakazoweza kutangaza fursa
mbalimbali ndani na nje ya nchi, hivyo kuongeza pato la Taifa.
“Tuendelee
kutafuta fursa za kuwainua na kunyanyua kazi za Tasnia yetu ya Filamu
ili waweze kunufaika na kufaidika na kazi zetu jambo litakalowezesha
kuijenga zaidi Tasnia ya Filamu,” amesema Waziri
Aidha,
Waziri amesisitiza Bodi kufuatilia utekelezaji wa uanzishaji wa Jumba
Changamani ambalo litakuwa maalum katika utengenezaji wa Filamu na
Michezo ya Kuigiza itakayowasaidia Wasanii kuandaa Filamu kwa urahisi na
zenye viwango bora zaidi.
Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbas amesisitiza Taasisi za Wizara
hiyo ikiwemo Bodi ya Filamu kufanya kazi kwa malengo ya kulinda na
kutetea maslahi ya Wanatasnia wa Filamu ili kuwawezesha kunufaika na
kazi zao za Filamu na Michezo ya kuigiza.
Kwa
upande wake Katibu Mtendaji Dkt. Kiagho Kilonzo akiwasilisha utendaji
wa Tasnia ya Filamu pamoja na majukumu ya Bodi hiyo amesema Tasnia hiyo
hadi kufikia mwaka 2021 imekuwa ikichangia katika kutoa ajira takribani
30,000 zinazotokana na shughuli za utayarishaji wa Filamu.
Ameongeza
kuwa Bodi hiyo tayari iko katika hatua za kuwa na Kanzidata yenye
taarifa za Wanatasnia wa Filamu kwa lengo la kutambua taarifa za
Wanatasnia wa Filamu kwa urahisi na usahihi zaidi.
Dkt.
Kilonzo amesema Bodi hiyo tayari inaendelea kuandaa mfumo wa Kidijitali
utakaosaidia kutoa huduma kwa Wanatasnia wa Filamu kwa urahisi bila
kufika Ofisini hapo. Aidha mfumo huo utarahisisha utoaji wa huduma kwa
Wanatasnia katika maeneo yao na kuwapunguzia gharama pamoja na kuwapa
uwezo zaidi wa kutekeleza majukumu yao.
No comments:
Post a Comment