Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt.
Selemani Jafo ametoa muda wa miezi sita kwa uongozi wa Bandari ya Mtwara
kufanyia marekebisho ya dosari za kimazingira zilizobainika.
Ametoa
maelekezo hayo Desemba 20, 2021 alipofanya ziara ya kikazi katika
bandari hiyo kwa ajili ya kufuatilia uzingatiaji wa Sheria ya Usimamizi
wa Mazingira ya mwaka 2004.
Dkt.
Jafo ameelekeza uongozi wa bandari hiyo kuandaa eneo maalumu
lililokidhi vigezo litakalotumika kuhifadhi makaa ya mawe
yanayosafirishwa baada ya kubaini yanahifadhiwa katika eneo lingine
lisilokidhi vigezo.
Hata
hivyo kwa kuanzia aliagiza kufanya ukaguzi wa kimazingira katika eneo
wanalotumia hivi sasa kuhifadhia makaa hayo mawe kwa kufuata utaratibu
wa sheria.
Alisema
bandari hiyo inafanya vizuri katika sekta ya uchukuzi na ina umuhimu
mkubwa kwa uchumi wa nchi hivyo inapaswa kuwa mfano bora wa kufuata
masharti yote ya mazingira yanayotakiwa.
“Tulitoa
cheti kwa ajili ya kuhifadhi makaa ya mawe na makaa haya ni heavy
metal, cheti kile hakitoki kama kadi ya harusi na ndio maana nilitaka
nikione. Bandari mlielekzwa mtenge eneo maalumu la kuyahifadhi lakini
mmeamua kwenda sehemu nyingine na watu wangu wa NEMC (Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira) waliwapiga faini, tunataka bandari
yetu ifanye vizuri kwa kufuata kanuni zilizowekwa na Serikali,”
alisisitiza.
“Binafsi
nafarijika kuona korosho zinasafirishwa kupitia bandari hii na hii
inaonesha namna miundombinu ya barabara inavyotunzwa na mnatoa ajira kwa
vijana wetu hapa na pia simenti inapitia hapa kwa hiyo uchumi unakua,”
alisema.
Kwa
upande wake Meneja wa Kanda ya Kusini, Mhandisi Boniface Guni alisema
bandari hiyo ilipata Cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira (EIA)
mwaka 2019 na kupewa masharti mbalimbali.
Miongoni
mwa masharti hayo ni kuweka miundombinu ya kudhibiti uchafuzi
unaotokana na maka ya mawe ikiwemo vumbi na maji ya mvua ambayo yanaweza
kuingia baharini pindi yakitiririka kwenye makaa hayo.
Meneja
Guni alibainisha hata hivyo eneo cheti kilichoelekeza bandari
haikutumia na badala yake ilianza kutumia eneo lingine ambalo kwa mujibu
wa cheti lina mapungufu.
Naye
Meneja wa Bandari ya Mtwara, Bw. Norbert Kalembo alisema wameyapokea
maelekezo ya Waziri Jafo yakiwemo kufanya ukaguzi wa kimazingira na
kuahidi kuyafanyia kazi.
Alisema Bandari ya Mtwara imekuwa ikijihusisha na shughuli za kupokea na kusafirisha makaa ya mawe, saruji na korosho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi
katika Bandari ya Mtwara Desemba 20, 2021 kwa ajili ya kufuatilia uzingatiaji
wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo (wa tatu kulia) akisikiliza maelekezo
kutoka kwa Meneja wa Bandari ya Mtwara, Bw. Norbert Kamlembo wakati wa ziara
yake ya kikazi katika Bandari ya Mtwara Desemba 2021. Wa pili kushoto ni Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara,
Dunstan Kyoba (wa pili kulia).Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika ziara ya kikazi katika Bandari
ya Mtwara Desemba 20, 2021 kwa ajili ya kufuatilia uzingatiaji wa Sheria ya
Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
No comments:
Post a Comment