MTIBWA SUGAR YAWAKUTA YA SIMBA SC - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 21, 2021

MTIBWA SUGAR YAWAKUTA YA SIMBA SC

 Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

KLABU ya Soka ya Mtibwa Sugar ya Morogoro imetoa taarifa ya kuumwa Mafua, Vifua na Homa Wachezaji wao takribani 15, Daktari wa timu na baadhi ya Viongozi wakati wakijiandaa mchezo wao wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBC Premier League) dhidi ya Polisi Tanzania uliopangwa kuchezwa Desemba 21, 2021 katika dimba la CCM Gairo mkoani Morogoro.

Kupitia Kocha wao, Awadhi Juma, Mtibwa wameeleza hali hiyo ilianza taratibu kwa Wachezaji hao huku idadi ya Wagonjwa ikiongezeka Kikosini hapo kadri muda unavyosogea, akiwepo yeye mwenyewe binafsi (Awadhi) kupatwa na maradhi hayo.

“Wachezaji wengi waliocheza mechi dhidi ya KMC FC pale Manungu, nusu yao wote wanaumwa, hatujui tatizo ni nini kila siku namba ya Wagonjwa kikosini inaongezeka, leo Golikipa wetu, Abuubakari Mshery amesema anajisikia vibaya, kwa kweli hatujui tatizo ni nini”, amesema Awadhi.

Awadhi amesema kuwa amesikia hali hiyo imewakuta wengi hapa nchini, ikiwa ni hali ya mabadiliko ya hali ya hewa kama ilivyoripotiwa na Wizara ya Afya nchini, kuwa ni hali ya kawaida kila mwaka (seasonal influenza). 

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) bado haijatoa taarifa wala maelekezo yoyote kuhusu hali hiyo iliyowakuta Mtibwa Sugar wakati wakijiandaa kuelekea kwenye mchezo huo dhidi ya Polisi Tanzania FC.

Hata hivyo, hali hiyo iliwakuta Wachezaji wa Simba SC waliopo mkoani Kagera kujiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar, mchezo uliokuwa uchezwe katika dimba la Kaitaba, Desemba 18, 2021 na mchezo huo uliahirishwa kutokana na hali hiyo.Kocha wa Mtibwa Sugar, Awadhi Juma akitoa taarifa ya kuumwa Wachezaji wao, Viongozi wa Benchi la Ufundi na Daktari wao, wakati wakijiandaa na mchezo dhidi ya Polisi Tanzania FC kwenye uwanja wa CCM Gairo, Morogoro.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad