MALEZI NA MAKUZI MEMA YA MTOTO NI MSINGI THABITI WA KUANDAA FAMILIA BORA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 20, 2021

MALEZI NA MAKUZI MEMA YA MTOTO NI MSINGI THABITI WA KUANDAA FAMILIA BORA

 

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Imeelezwa kuwa malezi na makuzi mema kwa Watoto ni msingi thabiti wa kuandaa familia bora na Taifa lenye viongozi waadilifu.

Kwa nyakati tofauti baadhi ya Wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wamesema kuwa Wazazi kutotimiza wajibu wao wa malezi na makuzi bora kwa watoto imekuwa ikichangia kuwa na viongozi wasiokuwa waadilifu tangu ngazi ya familia,hadi Taifa.

Wameeleza kuwa Vijana wanaotumia Dawa za kulevya,pamoja na Viongozi wapenda rushwa, wabadhirifu wa fedha,na rasilimali za Taifa ni matokeo ya Wazazi na Walezi kushindwa kutimiza wajibu wao wa malezi na makuzi mema kwa Watoto wao.

Wananchi hao wameshauri Wazazi na Walezi kuwekeza kwenye malezi na makuzi mema ya Watoto ili kuandaa familia Bora na viongozi waadilifu katika Taifa la Tanzania.

Wamesema familia zina wajibu mkubwa wa kuhakikisha watoto wanalelewa katika misingi imara ya dini zao ili waweze kuwa  na hofu ya Mungu.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad