HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 14, 2021

BENKI YA CRDB YAHITIMISHA MASHINDANO YA “CRDB BANK SUPER CUP” 2021 KWA KISHINDO JIJINI ARUSHA

Mashindano ya CRDB Bank Super Cup 2021 yaliyoshirikisha timu za wafanyakazi wa Idara na Matawi ya Benki ya CRDB nchi nzima, Tanzania Bara na Visiwani, yamehitimishwa leo jijini Arusha ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela. CRDB Bank Super Cup mwaka huu ilihusisha michezo ya mpira wa miguu kwa wanaume na mpira wa pete kwa wafanyakazi wanawake.

Kwa upande wa mpira wa miguu mashindano hayo yalishirikisha timu 16 za mpira wa miguu, kati ya hizo 8 ziliundwa kwa kushirikisha vitengo mbalimbali vilivyopo Makao Makuu ya Benki hiyo, na 8 zingine ziliundwa kutoka katika kanda mbalimbali ambazo zilitokana na Matawi yote ya Benki ya CRDB Tanzania nzima.

 Kwa upande wa wanawake timu 8 ziliundwa na kushiriki katika mchezo wa mpira wa pete zikijumuisha timu kutoka Makao Makuu na matawi. Timu zote zilipewa majina yatokanayo na bidha mbali mbali zinazotolewa na Benki hiyoikiwamo, timu za SimBanking, Tanzanite, Hodari, TemboCard, Nia Moja, Ulipo Tupo, nk.

Akizungumza malengo ya kuanzisha mashindano hayo ya “CRDB Bank Super Cup,” Mkurugenzi Mtendaji wa wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema, dhumuni kubwa la kuanzisha mashindano hayo ikiwa ni pamoja na burudani na kujenga afya ya mwili na akili kwa wafanyakazi, kuimarisha mahusiano baina ya wafanyakazi, pamoja na kuongeza uzalishaji kazini.

“Tunaamini mashindano haya ni hatua muhimu katika kufikia azma ya kuimarisha afya za wafanyakazi pamoja na kuongeza mshikamano na ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya kikazi ili kutoa huduma bora kwa wateja wao. Leo Tunahitimisha mashindano haya kwa mafanikio makubwa ikiwa ni mara ya kwanza mashindano haya kufanyika katika historia ya Benki yetu”. amesema Nsekela.

 Hitimisho la mashindano hayo liliambatana na utoaji wa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu na makombe kwa washindi mmoja mmoja na timu kwa ujumla. Mshindi wa kwanza alijinyakulia Shilingi Milioni 5 kwa mpira wa miguu na Shilingi Milioni 3 kwa mpira wa pete. Benki hiyo pia ilitoa zawadi kwa wachezaji binafsi waliofanya vizuri, ambapo mchezaji bora (Best Player) na mfungaji bora (Top Scorer) walipata Shilingi laki 2, na Shilingi laki 3 ilienda kwa mchezaji bora wa mechi ya fainali.

Nsekela aliwapongeza wafanyakazi wa Benki hiyo kwa kuitikia wito na kufanikisha mashindano hayo yaliyofana sana na kuleta upinzani baina ya timu shiriki hivyo kuleta chachu ya ubora wa ligi hiyo ya CRDB Bank Super Cup. “Huu ni mwanzo, mwaka ujao tutahakikisha tunayaboresha zaidi mashindano haya ikiwa pamoja na kuongeza timu za mpira wa kikapu katika ligi hii na kuongeza zawadi kubwa zaidi za washidi ili kuleta chachu za ushindani,” aliongezea Nsekela.

 

Naye Mkurugenzi wa Rasiliamali watu, Siophoro Kishimbo aliwashukuru Wakurugenzi wa Idara, Mameneja wa Kanda na Matawi wa Benki hiyo kwa kutoa ushirikiano wa kutosha na kuwapa wafanyakazi wao ruhusa ya kushiriki katika mashindano hayo. Alisema mashindano hayo yameleta chachu kubwa katika Benki na kuwapa fursa wafanyakazi weke kuonyesha vipaji walivyonavyo.

Benki ya CRDB imekuwa kwa kipindi kirefu ikiipa michezo umuhimu mkubwa hivyo kufikia kuendesha programu mbalimbali za michezo ikiwamo CRDB Bank Bonanza lilnalojumuisha timu za wabunge na wizara, CRDB Bank Marathon ambayo mwaka huu imepata usajili wa kimataifa, pamoja na mashindano ya taifa ya mpira wa kikapu “CRDB Bank Taifa Cup” ambayo yalifanyanyika mwezi Novemba mwaka huu yakishirikisha timu za kikapu za mikoa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad