AIRTEL NA LETSHEGO WACHEZESHA DROO YA KWANZA PROMOSHENI YA SHINDA NA TIMIZA AKIBA LEO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 16, 2021

AIRTEL NA LETSHEGO WACHEZESHA DROO YA KWANZA PROMOSHENI YA SHINDA NA TIMIZA AKIBA LEO

Meneja Uhusiao wa Airtel Tanzania Plc Jackson Mbando (kushoto), akiongea na mmoja wa washindi wa Droo ya kwanza ya Airtel Weka Akiba Ushinde na Timiza Akiba ambapo wateja wa Airtel Money watapata fursa ya kushinda hadi Tzs20, 000 kila wiki pale wanapoweka akiba kwenye akaunti ya Timiza Akiba na bila kutoa kwa wiki hiyo. kulia ni Meneja Chapa wa Airtel Tanzania Gillian Rugumamu, na katikati ni Mwakilishi wa Ofisi ya michezo ya kubahatisha Neema Tatu. 
 
 =====    =====    ======

Kampuni ya simu za mkononi Airtel kwa kushirikiana na benki ya Letshego leo wamechezesha droo ya kwanza ya promosheni ya Weka Akina Ushinde na Timiza Akiba leo ambapo wateja 25 wameibuka na zawadi ya shilingi elfu 20 kila mmoja katika akaunti zao za Airtel Money

akizungumza wakati wa droo hiyo Menejja wa Kitengo cha habari na Mahusiano Airtel Jackson Mmbando amesema wateja wote watawekewa hela leoleo na pia wayteja waendelee kuwekeza kwa kuwa bado kuna zawadi kubwa zaidi zitatolewa ikiwemo shilingi milioni 5 kwa mshindi wa kwanza, milioni 2 na laki 5 kwa mshindi wa pili pamoja na milioni moja mshindi wa tatu ambao watapatikana kwenye droo ya mwisho wa wiki ya sita kuanzia sasa.

Kampeni hii ina lengo la kuhamashisha utamanduni wa kuweka akiba kwa wateja wa Timiza Akiba na vile vile kuwavutia wateja wengine wapya. Tunaendelea kutoa wito kwa Watanzania kuendelea kujenga utamanduni wa kuweka akiba alisema Nchunda huku akiongeza kuwa Airtel Tanzania imeshirikiana na Letshego Bank kuendesha kampeni hii”.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad