Wiki ya masoko kufanyika Desemba Mosi hadi 3,2021 jijini Dar - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 23, 2021

Wiki ya masoko kufanyika Desemba Mosi hadi 3,2021 jijini Dar

Mkurugenzi wa Dentsu Aegis Network nchini, Edward Shilla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 23,2021 wakati akitambulisha wiki ya masoko ambayo itafanyika kuanzia Desemba Mosi hadi 3,2021. Kulia ni Mwanzilishi wa Inforcus Studio Ltd, Joshua Moshi na kushoto ni Mwanzilishi wa LAS consultancy, Salha Kibana. 

Mkurugenzi wa Dentsu Aegis Network nchini, Edward Shilla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 23,2021 wakati akitambulisha wiki ya masoko ambayo itafanyika kuanzia Desemba Mosi hadi 3,2021. Kulia ni Mwanzilishi wa Inforcus Studio Ltd, Joshua Moshi.
Mwanzilishi wa LAS consultancy, Salha Kibana akifafanua jambo wakati wa kutambulisha wiki ya Masoko itakayofanyika Regent business park on 172 Chwakustreet jijini Dar es Salaam Desemba Mosi hadi 3,2021. Katikati ni Mkurugenzi wa Dentsu Aegis Network nchini, Edward Shilla na Mwanzilishi wa Inforcus Studio Ltd, Joshua Moshi (Kulia)

KAMPUNI ya Masoko Kidigitali na Mawasiliano, Dentsu nchini, imezindua wiki ya masoko kwa lengo la kuwawezesha wataalamu wa fani ya Masoko, Mawasiliano na Mahusiano kuzibainisha na kuzitumia fursa zilizopo kwenye fani hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Novemba 23, 2021 Mkurugenzi wa Dentsu Aegis Network nchini, Edward Shilla amesema kuwa wiki ya masoko itafanyika kwa siku tatu kuanzia Desemba Mosi hadi 3,2021 Regent business park on 172 Chwakustreet ambapo pia kutakuwa na mijadala itakayoshirikisha wadau wa fani ya masoko na mawasiliano na kujadili njia za kufanya kazi kwenye fani hiyo.

Amesema kuwa Kauli mbiu ya mwaka huu inasema ” Takwimu kwenye uendeshwaji wa masoko” ambapo kati ya mambo yatakayogusiwa ni namna ambavyo takwimu inavyoweza kutumika kwenye kujenga haiba, Uwekezaji kwenye Vyombo vya Habari, Ubunifu katika Mawasiliano na kidigitali.

Shila amesema kwasasa matumizi ya data yamekuwa ni muhimu na yanatumika zaidi katika kutengeneza mazingira bora ya ufanisi wa kazi kwenye fani mbalimbali.

Hivyo hivyo hata kwenye fani hii ya masoko tunaweza kutumia data zilizopo katika kutengeneza mpango kazi mzuri wa shughuli za masoko na mawasiliano na kuzitumia vema fursa zinazopatikana.”

Akizungumzia tukio hilo Shilla amewashukuru wahisani wao ambao ni TBL, LAS consultancy, Eskimi, We media na infocus studio ambao wamefanikisha tukio hili licha ya hayo amewakaribisha wataalamu wote wa fani za masoko, mawasiliano kuhudhuria wiki ya Masoko.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad