Waziri
wa Nishati Mhe. January Makamba (kulia) akizungumza na Balozi wa Angola
Mhe. Sandro Renato Agostinho De Oliveira katika ofisi ndogo za Wizara
ya Nishati tarehe 25 Novemba, 2021 jijini Dar-es-salaam.

Waziri
wa Nishati Mhe. January Makamba akizungumza na Balozi wa Angola Mhe.
Sandro Renato Agostinho De Oliveira (Hayumo pichani) katika ofisi ndogo
za Wizara ya Nishati tarehe 25 Novemba, 2021 jijini Dar-es-salaam.

Waziri
wa Nishati Mhe. January Makamba (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na
Balozi wa Angola Mhe. Sandro Renato Agostinho De Oliveira katika ofisi
ndogo za Wizara ya Nishati tarehe 25 Novemba, 2021 jijini Dar-es-salaam
mara baada ya kumaliza mazungumzo.
**********************
Waziri
wa Nishati Mhe. January Yusuf Makamba amekutana na kufanya mazungumzo
na Balozi wa Angola nchini Tanzania Mhe. Sandro Renato Agostinho De
Oliveira kwa lengo la kujadili maeneo ya ushirikiano kati ya Tanzania na
Angola katika sekta ya nishati.
Mazungumzo
hayo yamefanyika leo tarehe 25 Novemba, 2021 katika ofisi ndogo za
Wizara ya Nishati jijini Dar-es-salaam wakiwemo wawakilishi kutoka pande
zote mbili za Tanzania na Angola.
Kupitia
kikao hicho, Waziri Makamba na Balozi Sandro Renato Agostinho De
Oliveira walijadili maeneo kadhaa ya ushirikiano katika sekta ndogo ya
mafuta na gesi asilia.
Maeneo
yaliyojadiliwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu katika masuala ya
biashara ya gesi iliyosindikwa (Liquefied Natural Gas – LNG); programu
za kujengeana uwezo kama vile mafunzo, warsha na makongamano;
uanzishwaji na uendeshaji wa hifadhi za kimkakati za bidhaa za petroli
(strategic petroleum reserves) na biashara ya mafuta.
Maeneo
mengine ya ushirikiano yaliyojadiliwa ni pamoja na kubadilishana
taarifa za fursa zilizopo katika biashara ya gesi ya kwenye mitungi
(Liquefied Petroleum Gas), viwanda vya petrokemikali; mitambo ya
kusafisha mafuta ghafi (refineries) na kubadilishana data na taarifa za
kitaalamu zinazohusiana na sekta ya mafuta na gesi asilia.
Katika
kuhitimisha, Waziri Makamba alieleza kuwa Tanzania ina mengi ya
kujifunza kutoka Angola hususan katika masuala ya mafuta kwani nchi hiyo
ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mafuta barani Afrika.
Kwa
mujibu wa takwimu, mwaka 2020 Angola ilishika nafasi ya pili kwa
uzalishalishaji wa mafuta barani Afrika ikitanguliwa na Nigeria.
Naye
Balozi wa Angola nchini alieleza kuwa ushirikiano wa Tanzania na Angola
utazinufaisha sana nchini hizi na kwamba Angola inaendela kujifunza
kutoka Tanzania kuhusu miradi mikubwa ya kimkakati ya mafuta na gesi
asilia ikiwemo mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima – Uganda hadi
Chongoleani Tanga – Tanzania na miradi ya usambazaji gesi asilia
inayotekelezwa nchini.
Tayari
Tanzania na Angola zimeanza mchakato wa kuwa na Mkataba wa Makubaliano
ya Awali (Memorundum of Understanding – MoU) itakayoongoza ushirikiano
wa nchi hizi katika sekta za madini, mafuta na gesi asilia tangu mwaka
2019.
No comments:
Post a Comment