HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 27, 2021

WAZIRI MAKAMBA AIHAKIKISHIA SHELL UTAYARI WA SERIKALI KUTEKELEZA MRADI WA LNG

Na Dorina G. Makaya - Dar-es-salaam.

WAZIRI wa Nishati Mhe. January Makamba tarehe 26 Novemba 2021, amekutana na Ujumbe kutoka Kampuni ya SHELL ulioongozwa na
Makamu wa Rais Mtendaji anaesimamia mradi wa kusindika gesi (LNG ) kwa upande wa Mashariki ( Africa, Asia na Australia) Bwana Cederic Cremers ambae amedhuru Tanzania kwa Mara ya Kwanza tangu kuchukua wadhifa huo mapema mwezi August 2021.

Katika ujumbe huo, bwana Cremers aliongozana na Makamu wa Rais na mkazi wa Shell Tanzania, bwana Jared Kuehl pamoja na mdau mwenzao bi Unni Fjaer kutoka kampuni ya Equinor.

Lengo la kikao hicho ni utambulisho wa Makamu wa Rais Mtendaji wa SHELL pamoja na kumhakikishia Waziri wa Nishati kuwa, Shell pamoja na Washirika wake wamejizatiti katika kuhakikisha mradi wa LNG unatekelezwa katika ufanisi, uwazi unaotakiwa na kwa wakati uliokusudiwa.

Waziri wa Nishati, ameuambia ujumbe kutoka Kampuni ya Shell kuwa, Serikali ya Tanzania ipo tayari kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati kwa manufaa ya pande zote mbili.

Waziri Makamba amebainisha kuwa, Serikali inautazama mradi wa LNG kwa mapana zaidi na kuwa, mradi wa kusindika gesi asilia ni mradi unaotarajiwa kuleta mabadiliko makubwa kiuchumi na kifedha pamoja na kuwajengea uwezo wazawa.

Aidha amesisitiza kuwa, pande zote mbili zihakikishe zinafanya haraka kuutekeleza mradi huu kwa wakati uliopangwa.

Pia Waziri Makamba amesema kuwa, yupo tayari kufanya kazi zaidi ili kuhakikisha dhima ya Serikali ya kukamilika kwa mradi huu inatekelezwa.
Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Shell, Cedric Cremers anayeshughulika na Masuala ya LNG Mashariki ya Mbali ( kushoto) alipofika. katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar-es-Salaam tarehe 26 Novemba, 2021 kwa lengo la kujitambulisha  kwa Waziri wa Nishati.
Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba (kulia) akiwa na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Shell, Cedric Cremers anayeshughulika na Masuala ya LNG Mashariki ya Mbali ( kushoto) alipofika. katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar-es-Salaam tarehe 26 Novemba, 2021 kwa lengo la kujitambulisha kwa Waziri wa Nishati.


Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Shell, Cedric Cremers  anayeshughulika na Masuala ya LNG Mashariki ya Mbali (wa pili kutoka kushoto) alipofika. katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar-es-Salaam tarehe 26 Novemba, 2021 kwa lengo la kujitambulisha  kwa Waziri wa Nishati.Wa kwanza kushoto ni Makamu wa Rais na Mwenyekiti Mkazi, Shell Tanzania Jared Keuhl na wa kwanza kulia ni Makamu wa Raisi na Mwenyekiti Mkazi, Equinor AS Unni Merethe Skorstad Fjær.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad