HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 5, 2021

WATUMISHI WAHIMIZWA KUWASILISHA MALALAMIKO YAO KULIKO KUPITA NJIA ZA MKATO

 

Na Mwandishi Wetu - Michuzi Tv
WIZARA ya mambo ya ndani ya nchi imewaagiza watumishi wake kufuata utaratibu katika kuwasilisha malalamiko yao badala ya kupita njia za mkato.

Agizo hilo lilitolewa leo November 5, 2021 na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Athuman Kailima wakati akifungua Baraza dogo la wafanyakazi wa Wizara hiyo.

Kailima alikemea kitendo cha baadhi ya watumishi kutoa taarifa za malalamiko katika maeneo yasiyohusika kwamba kinachangia kuvujisha Siri za Wizara na kufanya mambo mengi kuonekana nje ya utaratibu.

Naibu Katibu Mkuu alisema watumishi wengi wamekuwa wakipeleka malalamiko yao kwa njia zisizokuwa sahihi kitendo alichosema ni kibaya kwa utumishi wa umma.

"Kikubwa tunasisitiza utunzaji wa siri,taarifa yoyote ikipelekwa mahali pasipohusika ni kuwa imevuja, na hili la malalamiko nasisitiza lifuate utaratibu mzuri kuepusha taarifa kwenda kusikohusika," alisema Kailima.

Katika hatua nyingine kiongozi huyo amesema korona bado ipo hivyo watu wachukue tafadhari ikiwemo kuongeza kasi ya uchanjaji.

Mwenyekiti wa baraza hilo Emanuel Kayuni alisema lengo la kuanzisha mabaraza hayo ni pamoja na kukumbushana wajibu wao na haki mahali pa kazi.

Kayuni alisema baraza lina wajumbe 67 ingawa jana walishiriki wajumbe 58 akisema wamejiandaa kuwekeana mikakati ya kuwapeleka mbele.

Jeniva Ndonde alisema maelekezo ya Naibu Katibu Mkuu ni dira inayoweza kuwasukuma kwenda mbele ya mahali walipo.

Jeniva alisema baraza ni mwakilishi wa watumishi wengine hivyo watakwenda kuwaambia na kupeana mikakati ya pamoja ili kufikia malengo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad