HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 22, 2021

Watanzania wamehimizwa kuwekeza katika Kilimo cha Vanilla

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vanilla International, Simon Mnkondya katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na Zao la Vanilla na jinsi linavyotajilisha watu na nchi.

WATANZANIA wamehimizwa kuwekeza katika Kilimo cha Vanilla ili waweze kujikwamua kwa kupata kipato kitakachoweza kuwainua na kuinua uchumi wa nchi kwa ujumla.

Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanilla Internation  inayojishughulisha na kilimo cha Vanilla, Simon Mnkondya wakati akizungumza na waandishi habari Jijini Dar es salaam, amesema asilimia 90 ya watanzania wengi wamejiajiri katika sekta nzima ya Kilimo.

Amesema fursa ya Kilimo ndio pekee ambapo wananchi wanauwezo wa kufaidika zaidi kwa kujikwamua kiuchumi na kuiwezesha nchi kuweza kwenda mbele zaidi.

"Kilimo cha Vanilla ni Kilimo ambacho kipo katika Kilimo Biashara kwani kilo moja ya zao hilo huuzwa kwa shilingi Millioni moja na pia ni miongoni mwa zao ambalo linakubalika katika mataifa ya nje. " Amesema

Amesema Kilimo cha zao la Vanilla ni miongoni wa fursa ambayo ni adhimu na inayohitajika duniani hivyo jamii ikijikita katika kilimo hicho inaweza kujikwamua kiuchumi.

Mnkondya ambaye pia ni mwamzilishi wa Taasisi hiyo alisema katika kutambua fursa  zilizopo katika Kilimo cha Vanilla Taasisi hiyo  iliamua kuwekeza zaidi katika zao hilo ambapo iliweza kubaini fursa mbalimbali zilizopo katika zao hilo

Amesema kampuni iliamua kuanzisha mradi  katika Mkoa wa Iringa ambapo huko hutoa fursa kwa wakulima  kuwekeza kwa ajili ya Kilimo hicho na badae kupata masoko kupitia kampuni hiyo hiyo.

Mndya amesema kuwa  wameanzisha mradi wa kilimo cha Vanilla ambapo wanatoa fursa kwa wakulima kuwekeza na badae kupata fursa ya kuwatuzia zao hilo la vanilla na kusisitiza kuwa kampuni hiyo inanunua zao hilo kwa mkulima ambaye tayari amejisajili katika kampuni hiyo. 

Mbali na hilo pia Mnkondya amesema Kampuni hiyo imefanikiwa kutoa  ajira kwa vijana wakike ambao wamezalishwa watot na kutelekezwa ili waweze kujikwamua katika maisha yao kwa kupata kipato.

"Asilimia 60 ya wafanyakazi katika kampuni yetu ni wasichana ambao wametelekezwa na wanaume zao ambapo kwa mujibu wa utafiti tulioufanya tumebaini wanasichana hawa ni wavumilivu Sana. "Amesema Mnkondya

Akizungumza kuhusu kwanini mradi huo upo katika mkoa wa Njombe Mnkondya amesema Kampuni hiyo ilifanya tafiti katika baadhi ya mikoa na kubaini zao  la Vanila limekuwa likiitaji ardhi ambayo inaendana na kilimo hicho.

Aidha alitoa wito kwa watanzania na wakulima kwa ujumla kwenda kutembelea mradi huo ili waweze kujifunza fursa mbalimbali na kuwekeza katika Kilimo cha Vanilla, licha ya hayo alibainisha mikoa ambayo zao la Vanilla linastawi kuwa ni Bukoba, Njome, Iringa, Mbeya na Moshi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vanilla International, Simon Mnkondya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na Zao la Vanilla na jinsi linavyotajilisha watu na nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad