Joto la mashindano ya kimataifa ya urembo ya Miss East Africa 2021 limeanza kupanda ambapo washiriki wa mashindano hayo wataanza kuingia Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii.
Makamu wa Rais wa mashindano hayo,
Jolly Mutesi amesema washiriki hao wapo tayari kwa maandalizi ya mwisho
ambapo fainali ya mashindano hayo yanayosubiliwa kwa hamu kubwa
itafanyika Desemba 17, 2021 katika ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es
salaam
Amesema kwamba msanii Mboso wa Tanzania ni mmoja wa
wasanii wakubwa watakaotumbuiza katika mashindano hayo yanayotarajiwa
kuangaliwa na mamilioni ya watu barani Afrika LIVE kupitia katika
Television na Internet Duniani kote.
Nchi zinazoshiriki mashindano ya Miss East Africa ni pamoja na Kenya, Uganda,
Rwanda, South Sudan na Somalia. zingine ni Reunion, Ethiopia, Malawi, Burundi na Mauritius.
Kiingilio cha chini katika mashindano hayo ni Tsh 50,000 kwa tiketi za kawaida na Sh100,000 kwa VIP na Tsh200,000 kwa VVIP
Mashindano
ya Miss east Africa yanaandaliwa na kampuni ya Rena Events kwa
kushirikiana na Wasafi Media.“Tanzania itawakilishwa na Mrembo Queen
Mugesi ambae aliwashinda warembo zaidi ya 2,600 wa Tanzania walioomba
kuiwakilisha nchi kwa njia ya mtandao ambapo Queen Mugesi alichaguliwa
katika mchakato ulioendeshwa na wataalamu wa mambo ya urembo kwa zaidi
ya mwezi mmoja,” alisema.
Alisema, mashindano ya Miss East Africa
ambayo yaliasisiwa na Mtanzania Rena Callist mwaka 1996, yanasubiriwa
kwa hamu kubwa na wapenzi wa mambo ya urembo na yanatarajiwa kuangaliwa
na zaidi ya watu milioni 200.
No comments:
Post a Comment