HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 11, 2021

VIVO ENERGY YARUDISHA VILAINISHI VYA SHELL TANZANIA

Wadau na wasambazaji wa mafuta kutoka kampuni ya Vivo Energy wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Vilainishi vya Shell hapa nchini.
Kutoka kushoto ni Meneja Mkuu wa Ufundi wa Vivo Energy, Fred Omondi, Mkurugenzi Mkuu wa Vivo Energy Tanzania, Khady Sene, Meneja wa Biashara wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Kemilembe wengine ni meza kuu wakiwa katika uzinduzi wa Vilainishi vya Shell hapa nchini, uzinduzi uliofanyika hoteli ya Hyatt Regency jijini  Dar es Salaam Novemba 10,2021.
Mkurugenzi Mkuu wa Vivo Energy Tanzania, Khady Sene akizungumza wakati wa uzinduzi wa kurudisha Vilainishi vya Shell hapa nchini, uzinduzi huu umefanyika Hoteli ya Hyatt Regency jijini  Dar es Salaam Novemba 10,2021.


KAMPUNI ya VIVO ENERGY wauzaji wa vilainishi vya Shell na mafuta hapa nchini wamerejesha na  kuzindua rasmi vilainishi vya Shell katika soko la Tanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Novemba 10, mwaka huu  jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Vivo Energy Tanzania, Bibi Khady Sene amesema kuwa, lengo la Kampuni hiyo ni kufikisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu barani Afrika.

Amesema kuwa Vivo Energy wameshirikiana na Kampuni nambari moja ya vilainishi duniani ya Shell kurudisha vilainishi vyake nchini Tanzania.

“Kampuni ya Shell kwa zaidi ya karne ya ishirini imekuwa chapa inayotambulika zaidi ulimwenguni. Miongo kadhaa ya juhudi imeingia katika kuanzisha sifa ya chapa yetu kwa bidhaa bora na huduma ambazo wateja wanaweza kuamini. Leo, Shell ndio wasambazaji nambari moja wa vilainishi duniani, wakiwasilisha vilainishi vinavyoongoza sokoni kwa wateja katika zaidi ya nchi 100. Vilainishi vya Shell huleta maarifa ya kiteknolojia ya kiwango cha juu kwa bidhaa zake, na kutoa uundaji bora zaidi wa magari." Amesema.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Ufundi wa Vivo Energy, Fred Omondi amesema kuwa Vilainishi vya Shell vinawapa wateja kutoka Bara la Afrika viwango vya juu kwaajili ya ulinzi, utendaji na ufanisi wa injini za magari, na injini za pikipiki visivyopatikana kwingineko.

Omond amewahakikishia watanzania usalama wa vilainishi hivyo katika soko la Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Akimwakilisha Mkurugenzi mtendaji , Meneja wa Biashara wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Kemilembe Kafanabo amesema urejeshaji wa vilainishi vya Shell utaleta ushindani katika soko pamoja na kutambulika kwa kampuni ya Vivo Energy kama wasambazaji wakuu wa vilainishi hivyo.

Ameeleza kuwa, EWURA wataendelea kusajili vilainishi pamoja na kampuni zote zinazosambaza vilainishi kote nchini.

"Vivo Energy wanatambulika katika Usambazaji wa vilainishi halisi vya Shell lubricants katika soko la Tanzania, ni hatua nzuri katika kukuza uchumi wetu na sekta ya nishati kwa ujumla." Amesema.

Kemilembe ameipongeza kampuni hiyo kwa kuendelea kusogeza huduma zao zaidi kwa nchi za Afrika ambapo hadi sasa wanatoa huduma zao kupitia shell Lubricants kwa nchi zipatazo 23.

Meneja wa Biashara wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Kemilembe Kafanabo akizungumza wakati wa kutambulishwa Vilainishi vya Shell hapa nchini katika uzinduzi uliofanyika hoteli ya  Hyatt Regency jijini  Dar es Salaam Novemba 10,2021.
Meneja Mkuu wa Ufundi wa Vivo Energy, Fred Omondi akizungumza wakati wa kutambulishwa Vilainishi vya Shell hapa nchini katika uzinduzi uliofanyika hoteli ya Hyatt Regency jijini  Dar es Salaam Novemba 10,2021.
Kutoka kushoto ni Meneja Mkuu wa Ufundi wa Vivo Energy, Fred Omondi, Mkurugenzi Mkuu wa Vivo Energy Tanzania, Khady Sene, Meneja wa Biashara wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Kemilembe wengine ni meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa na picha ya vidumu vya vilainishi mbalimbali ambayo ni vya kampuni ya Shell vitakavyosamazwa na Kampuni ya Vivo Energy.



Picha za mapoja za wadau wa mafuta hapa nchini wakati wa uzinduzi wa Vilainishi vya Shell hapa nchini.
Picha ya pamoja.


Wadau wa Mafuta hapa nchini wakiangalia uzinduzi wa Vilainishi vya Shell hapa nchini.


Watumbuizaji kutoka Nyumba ya Vipaji Tanzania(THT) wakitumbuiza katika uzinduzi wa Vilainishi vya Shell hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad