EQUITY BANK (T) NA SHIRIKA LA POSTA WAKUBALIANA KUTUMIA VITUO VYA SHIRIKA LA POSTA KUTOA HUDUMA ZA KIBENKI ILI KUFIKISHA HUDUMA ZA KIFEDHA KARIBU ZAIDI NA WANANCHI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 11, 2021

EQUITY BANK (T) NA SHIRIKA LA POSTA WAKUBALIANA KUTUMIA VITUO VYA SHIRIKA LA POSTA KUTOA HUDUMA ZA KIBENKI ILI KUFIKISHA HUDUMA ZA KIFEDHA KARIBU ZAIDI NA WANANCHI


Benki ya Equity (T)
imetia saini Mkataba wa Makubaliano na Shirika la Posta nchini kutumia
ni vituo vya Shirika hilo kutolea huduma zake za kibenki ili kusogeza
huduma karibu zaidi na wateja wake na watanzania kwa ujumla.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba huo jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Robert Kiboti
amesema kuwa kupitia mtandao wa Ofisi za Shirika la Posta nchini ,
Benki ya Equity itaweza kuwafikia maelfu ya wananchi nchi nzima na
kuwapatia huduma bora zaidi za fedha. “Hatua hii itatuongezea wigo wa
mtandao wa utoaji huduma zetu ambazo ni nafuu zaidi nchini na hivyo
kuendana na lengo letu la kukomboa Watanzania kiuchumi kwa
kuongeza ushiriki wa mfumo rasmi wa fedha (financial inclusion).
“Kwa sasa Equity Bank ina mawakala wapatao 3,900 na hivyo kuungana
na Shirika la Posta kuwa kama Supa Wakala wetu , kupitia mtandao wa
ofisi zake 35, kutatuwezesha kuongeza idadi ya wananchi
watakaofikiwa na huduma zetu kwa ukaribu na urahisi zaidi. Kwa
kuanzia tutaanza na vituo 35 kwa maeneo kama Karatu, Namanga,
Tegeta, Geita, Iringa Mjini, Mafinga, Bukoba, Katavi, Kasulu, Rombo,
lindi, Babati, Tarime, Njombe, Rukwa, Makambako, Chalinze,
Sumbawanga, Songea, Nzega, Singida, Tanga na Pemba” alisema.
Kiboti amesema kuwa ushirikiano huo ni utekelezaji wa sera ya Benki ya
Equity ya kuwakomboa wananchi kiuchumi kwa kuwapa huduma nafuu
za kifedha. “Akaunti zetu hazina makato ya mwezi na tuna viwango bora
kabisa vya riba sokoni. Pia kupitia vituo hivi vipya huduma nyingi
zitatolewa ikiwemo kufungua akaunti, kulipa ankara na kutoa floti kwa
Mawakala wodog0 waliopo karibu” amesema Kiboti.
Kwa upande wake, Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta
Tanzania, Macrice Mbodo amesema kwa kuanza shirika hilo na Equity
Bank wataanza kutoa huduma katika ofisi zake 35 zilizo maeneo
mbalimbali nchini. “Tunajivunia kuweza kuungana na Benki ya Equity
katika kufanikisha mpango huu utakaosaidia kufikisha huduma za
kibenki kwa Watanzania wengi zaidi. Juu ya hilo kupitia mpango huu
Shirika la Posta pia litapata chanzo kipya cha mapato kupitia kamisheni
na hivyo kuimarisha mapato ya shirika”. Amesema.
Benki ya Equity imekuwa kinara wa kutumia mifumo ya kidijitali kutolea
huduma zake huku ikiongoza kwa ufanisi wa njia mbadala za kutolea
huduma ikiwemo Mawakala. Kwa sasa, zaidi ya asilimia 85 miamala
yote ya wateja wa Benki ya Equity imekuwa ikifanyika nje ya Matawi
kupitia huduma mbadala na kidijitali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Robert Kiboti akitia saini Mkataba wa Makubaliano na Shirika la Posta nchini kutumia
ni vituo vya Shirika hilo kutolea huduma zake za kibenki ili kusogeza
huduma karibu zaidi na wateja wake na watanzania kwa ujumla.saini Mkataba wa Makubaliano na Shirika la Posta nchini kutumia
ni vituo vya Shirika hilo kutolea huduma zake za kibenki ili kusogeza
huduma karibu zaidi na wateja wake na watanzania kwa ujumla.
 Kutoka kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Robert Kiboti na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta
Tanzania, Macrice Mbodo Wakikabidhiana Mkataba
Mkataba wa Makubaliano na Shirika la Posta nchini kutumia ni vituo vya Shirika hilo kutolea huduma zake za kibenki ili kusogeza huduma karibu zaidi na wateja wake na watanzania kwa ujumla.saini Mkataba wa Makubaliano na Shirika la Posta nchini kutumia ni vituo vya Shirika hilo kutolea huduma zake za kibenki ili kusogeza huduma karibu zaidi na wateja wake na watanzania kwa    ujumla.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Robert Kiboti akizingumza na wageni mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari katika zoezi la kutia saini  Mkataba wa Makubaliano na Shirika la Posta nchini kutumia ni vituo vya Shirika hilo kutolea huduma zake za kibenki ili kusogeza huduma karibu zaidi na wateja wake na watanzania kwa ujumla.saini Mkataba wa Makubaliano na Shirika la Posta nchini kutumia ni vituo vya Shirika hilo kutolea huduma zake za kibenki ili kusogeza huduma karibu zaidi na wateja wake na watanzania kwa    ujumla.
 Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta
Tanzania, Macrice Mbodo akizungumza na vyombo vya habari nchini


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad