HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 11, 2021

TRA TANGA YAWAFIKISHA MAHAKAMANI WAFANYABIASHARA SITA KWA KOSA LA KUKWEPA KODI YA SERIKALI

 Afisa Sheria kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania Octavian Joseph Chenje akizungumza na waandishi wa habari


Afisa Kodi na Msimamizi wa Kitengo cha Mashine za EFD Mkoa wa Tanga Teofil Ngambeki akizungumza na waandishi wa habari kulia ni Afisa Sheria kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania Octavian Joseph Chenje

NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
MAMLAKA ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Tanga imewafikisha mahakamani wafanyabiashara sita kwa kosa la kukwepa kodi ya serikali kwa kutokutoa risiti za EFD Mashine.

Mashauri hayo sita yanayohusisha wafanyabiashara hao yamefikishwa kwa mara ya kwanza mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga yanayohusisha kutokutii matakwa ya kisheria ya kutumia mashine za EFD ikiwa ni pamoja na kutokutoa risiti za mauzo ambayo wanayafanya.

Mashauri hayo ambayo bado yako kwenye hatua za awali yameahirishwa mpaka November 29 na Mengine December 7 kutokana na sababu mbali mbali na watuhumiwa wako nje kwa dhamana.

Akizungumza na waandishi wa Habari nje ya Mahakamana Afisa Sheria kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania Octavian Joseph Chenje alisema amekuja Tanga kwa ajili ya kesi mbalimbali zinazohusiana na matumizi ya mashine za kutolea risiti yaani EFD na walikuwa na mashauri sita kwenye mahakama ya hakimu mkazi Tanga.

Alisema masahuri yenyewe yanahusu masuala la utii matakwa ya sheria ya kutumia mashine za EFD ikiwemo pamoja na kutoa risiti kwa mauzo ambayo wanakuwa wakifanya .

Aidha alisema wapo baadhi ya wafanyabiashara ambao wameomba kulipa faini kutokana na makosa yao hivyo watalishughulikia suala lao na watakaa kama TRA na waendesha mashtaka ya TRA kuweza kuona kama watafanyia kazi maombi yao au waendelee na kesi.

Mwanasheria huyo alisema aliwataka wafanyabiashara kutii sheria bila shuruti sheria yua kodi ya mwaka 2015 ya usimamizi wa kodi inamtaka kila mfanyabiashara kuwa na mashine za EFD na usipofanya hivyo ukitamatwa mkono wa sheria utachukua hatua zake.

Mtu ambaye hakutoa risiti kwa mujibu wa sheria ni faini ya milioni 3 hadi Milioni nne na nusu au adhabu hiyo pamoja na kifungo kisichozidi miaka miwili .

Naye kwa upande wake Afisa Kodi na Msimamizi wa Kitengo cha Mashine za EFD Mkoa wa Tanga Teofil Ngambeki alisema wanajitahidi kuwaelimisha wafanyabishara kufanya biashara zao wafuate sheria za kodi pale ambapo mtu ameuza kwa kutoa risiti.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad