Waziri wa Ujenzi na uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amewaagiza wakuu
wa Taasisi za usafiri wa anga nchini kuhakikisha kila mtumishi aliyepo
au anayefanya kazi kwenye viwanja vya ndege, Mashirika ya ndege na watoa
huduma wengine kutii na kufuata taratibu za kiusalama zilizopo kwa
mujibu wa miongozo ya kitaifa na kimataifa.
Rai hiyo ameitoa mapema leo wakati akihutubia katika uzinduzi
wa mwaka wa Utamaduni wa Usalama wa Usafiri wa Anga (YEAR OF SECURITY
CULTURE - 2021) iliyofanyika Makao makuu ya Mamlaka ya Anga Tanzania
(TCAA) jijini Dar es Salaam.
Prof.
Mbarawa amesema kuwa suala la usalama katika viwanja vya ndege ni
muhimu kuzingatiwa kwani bila kutiliwa mkazo linaweza kuleta maafa
makubwa.
"Viongozi naomba mtilie mkazo swala
la ukaguzi halina msamaha isipokuwa kwa viongozi wakuu wa nchi
wanaomtambulika kisheria. Kukataa au kukaidi kukaguliwa ni kukiuka
sheria za nchi na za Kimataifa," Amesema Prof. Mbarawa.
Amesema
kuwa usafiri wa anga ni salama kuliko njia nyingine zote za usafiri
duniani. Usalama huu wa usafiri wa anga ni mafanikio makubwa ambayo
hayatokei yenyewe, bali kwa jitihada mbali mbali zinazofanywa na
wataalam wa usafiri wa anga hapa nchini na duniani kwa ujumla kwa
kushirikiana pamoja kuweka mifumo na kanuni za uendeshaji na usimamizi
wa shughuli zote za usafiri wa anga.
"Pamoja
na jitihada hizi, ni wazi kwamba suala la usalama wa anga (Aviation
Security) limekua na changamoto duniani kote zitokanazo na uwepo wa
matishio au matendo ya kigaidi kwa kipindi fulani na wakati mwingine
kurudi katika hali ya kawaida au kuonekana kuwa katika hali ya kawaida
kinyume na uhalisia. Changamoto hii imepelekea madhara kadhaa duniani
ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha ya wasafiri wa ndege na hata
wasiosafiri, uharibifu wa mali na miundombinu, kuzorota kwa shughuli za
utalii na biashara duniani kutokana na hofu ya vitendo vya kigaidi dhidi
ya usafiri wa anga. Kutokana na hali hii, mbinu za kukabiliana na
changamoto hizi zinapaswa kuwa endelevu na shirikishi ili ziweze kuwa na
tija," Amesema.
Amesema
mwaka 2021 ni mwaka muhimu katika historia ya usalama wa usafiri wa
anga kwani ndio kumbukizi ya miaka 20 ya tukio la utekaji nyara wa ndege
4 za abiria ambazo hatimae zilitumika kama silaha kwa magaidi
kutungulia majengo mawili ya kibiashara na jengo la makao makuu ya
wizara ya ulinzi nchini Marekani. Tukio hili maarufu kama 9/11 ,(yaani
11 Septemba 2001) lilipelekea vifo vya maelfu ya watu waliokuwa ndani ya
ndege hizo pamoja na majengo yaliyotunguliwa na ndege hizo. Mbali na
vifo hivyo, zilijitokeza athari nyingi sana kiuchumi na hata kijamii
duniani kote mpaka sasa. Hali hii inatukumbusha kwamba, Usalama ni
wajibu wa kila mtu, kila nchi na hata taasisi moja moja, kwani bila
kujali tukio limetokea wapi na nani amesababisha, madhara ya tukio hilo
yatatufikia sote.
Kwa
upande wake Mkururgenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania
(TCAA), Hamza Johari ametilia msisitizo na kuahidi kulisimamia suala a
ukaguzi katika viwanja vya ndege na kutoa wito kwa watendaji wengine
kutona kero pindi wanapolazimika kukaguiwa.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa mwaka wa utamaduni wa usalama wa usafiri wa anga uliofanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa AngaTanzania (TCAA).

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa akikaguliwa kama sehemu ya Uzinduzi wa mwaka wa utamaduni wa usalama wa usafiri wa anga uliofanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Profesa Makame akifuatiwa na baadhi ya watendaji wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kukaguliwa ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa mwaka wa utamaduni wa usalama wa usafiri wa anga.
Waziri
wa Ujenzi na uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akizungumza katika uzinduzi
wa mwaka wa Utamaduni wa Usalama wa Usafiri wa Anga (YEAR OF SECURITY
CULTURE - 2021 ) iliyofanyika Makao makuu ya Mamlaka ya Anga Tanzania
(TCAA) jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa mwaka wa utamaduni wa usalama wa usafiri wa anga uliofanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa AngaTanzania (TCAA).

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa akikaguliwa kama sehemu ya Uzinduzi wa mwaka wa utamaduni wa usalama wa usafiri wa anga uliofanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Profesa Makame akifuatiwa na baadhi ya watendaji wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kukaguliwa ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa mwaka wa utamaduni wa usalama wa usafiri wa anga.
Mkururgenzi Mkuu – Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari akizungumza katika uzinduzi wa mwaka wa Utamaduni wa Usalama wa Usafiri wa Anga (YEAR OF SECURITY CULTURE - 2021 ) iliyofanyika Makao makuu ya Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment