Ecobank
Tanzania imeshiriki maonesho ya Wiki ya huduma za Fedha Kitaifa ili
kuongeza uelewa kwa wananchi kwa lengo la kuchochea ustawi kwa Maendeleo
ya Kijamii yenye Kauli mbiu ya “Boresha Maisha kupitia elimu ya fedha.”
Maadhimisho
hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango yameanza toka Novemba
08 hadi Novemba 14 mwaka huu yanalenga wadau mbalimbali wakiwemo;
watumishi wa umma, wanafunzi, wakufunzi, wanawake, vijana, watu wenye
mahitaji maalumu; wajasiriamali wadogo na wa kati (MSMEs); asasi za
kiraia; Wahariri na waandishi wa vyombo vya habari; watoa huduma za
fedha; na umma kwa ujumla.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Fedha na Mipango wa Zanzibar, Jamal Kassim Ali amesema Serikali imepanga
kutumia Fedha kwenye mitaji ya wajasiriamali wadogowadogo ambao wanatoa
huduma za kifedha kwenye Mpango wa Maendeleo ya sekta ya Fedha hapa
nchini.
Amesema
Elimu ijikite kwenye huduma za Fedha ili waweze kukuza kipato cha mtu
mmojamoja na kuongeza mapato kwa taifa hivyo ni vyema kujipima ipasavyo
ili kuongeza ufanisi kwenye huduma za kifedha hapa nchini.
Naye
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Masoko na Mawasiliano Ecobank
Furaha Samalu amesema Benki hiyo imeshiriki katika maonesho hayo ili
kuweza kitangaza huduma wanazozitoa ili kuweza kupanua wigo kwa wananchi
hasa wajasiriamali wadogowadogo.
Poa
amesema Ecobank Tanzania wanatoa huduma za kifedha kama vile kufungua
akaunti, huduma ya benki kwa njia ya wakala, kubadili Fedha za kigeni,
bima pamoja mikopo pamoja na huduma ya Ellevate kwa ajili ya kuinua
Biashara zinazowahusu wanawake hii yote ikiwa ni kuwafikia wananchi wote
na kutoa huduma iliyobora.
Amewakaribisha
wananchi kutembelea Banda la Ecobank Tanzania ili kuweza kupata elimu
ya kifedha kutoka kwenye benki hiyo kwenye maonesho ya wiki ya Huduma za
Fedha Kitaifa.
Afisa
Mauzo wa Ecobank Tanzania, Neema Mbiru(kushoto) kitoa elimu kuhusu
huduma zinazotolewa na benki hiyo kwenye maonesho ya Wiki ya Huduma za
Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es
Salaam leo.
Afisa
Mauzo wa Ecobank Tanzania Neema Yonah Kondowe(kulia) akitoa ufafanuzi
kuhusu akaunti za watoto kwa mmoja wa wananchi waliotembelea Banda la
Ecobank Tanzania kwenye maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa
yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam leo
yaliyozinduliwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa
Zanzibar, Jamal Kassim Ali.
Maafida
mauzo wa Ecobank Tanzania wakigawa vipeperushi mara baada ya kutoa
elimu kwa wananchi waliofika kwenye Banda la Ecobank Tanzania wakati wa
maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja
vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam leo.
Elimu ikiendelea kutolewa kwenye Banda la Ecobank Tanzania leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Huduma kwa Wateja, Masoko na Mawasiliano Ecobank Tanzania, Furaha
Samalu(kushoto) pamoja na na Mkuu wa Kitengo cha Masoko Ecobank
Tanzania Juma Hamisi(kulia) wakiwa kwenye Bada la Benki hiyo wakati wa maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment