HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 4, 2021

TANZANIA HAIJATOA KATIKA MAHAKAMA YA AFRIKA- DKT MPANGO

 SERIKALI imesema, Tanzania haijajitoa katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu bali imejiondoa katika tamko lililofanywa chini ya ibara ya 34 (6) ya itifaki ya uanzishwaji wa Mahakama hiyo inayoruhusu mashirika yasio ya kiserikali pamoja na watu binafsi kuishitaki serikali katika mahakama hiyo.


Amesema Tanzania itaendelea kushirikiana vema na mahakama za Afrika kwa kutambua kwamba Afrika inahitaji vyombo vyake vya utoaji haki katika kutatua changamoto za waafrika.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango wakati akifungua Mjadala wa Tano wa Umoja wa Afrika unaohusu Mahakama uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere Dar es salaam. Mjadala huo umebeba kauli mbiu ya kujenga imani ya wananchi kwa Mahakama Barani Afrika.

Amesema ni muhimu kwa kwa Mahakama za Afrika kufahamu sababu zinazopelekea wananchi kupoteza Imani na mahakama hizo ili kuzifanyia kazi na kuziondoa changamoto hizo.

"Wananchi wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali wakati wa kutafuta haki zao katika mahakama ikiwemo ucheleweshaji kesi kuhairishwa mara nyingi, kutumika kwa lugha za kigeni katika utoaji hukumu, kuchelewa kwa utekelezaji wa hukumu, amapo kanuni zinasema haki ikicheleweshwa ni kunyimwa haki inabaki kuwa kilio." Amesema Dkt. Mpango

Amesema katika kuongeza Imani kwa wananchi mahakama zinapaswa kuweka mkazo katika kudhibiti Rushwa ili kutoa usawa kwa wananchi wote kupata haki zao.

Pia ametoa wito kwa mahakama kuongeza matumizi ya Tehama katika shughuli zake ili kuongeza uwazi na urahisi wa kufikika na kusimamia uhuru kuondoa upendeleo katika utoaji haki, ni muhimu majadiliano hayo yakatafuta suluhu na kutoa mapendekezo sahihi ya uelekeo wa Mahakama.

Kwa upande wake Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jaji Imani Aboud amesema kuongezwa kwa ufanisi katika utaoaji haki katika mahakama za ndani kwa nchi wanachama wa mahakama ya Afrika kutapunguza mrundikano wa kesi.

Amesema mdahalo wa siku mbili utaongeza ufanisi wa utaoaji haki pamoja na kulinda haki za binadamu katika mahakama za ndani ya nchi.


Akizungumza kwa niaba ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji wa mahakama kuu ya Tanzania kitengo cha Biashara, Dkt. Deo Nangela, amesema imani kwa mahakama inaongeza Amani na utulivu katika nchi inayopelekea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Amesema Tanzania imeendelea kuboresha mifumo ya Tehama katika utoaji haki na kuongeza kwamba umuhimu wa matumizi yake unazidi kuonekana hasa wakati kipindi hiki cha mlipuko wa Uviko 19.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na washiriki wakati wa ufunguzi wa Mjadala wa Tano wa Umoja wa Afrika unaohusu Mahakama uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Novemba 4, 2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akikabidhiwa zawadi na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jaji Imani Aboud mara baada ya ufunguzi wa Mjadala wa Tano wa Umoja wa Afrika unaohusu Mahakama leo Novemba 4,2021.
Baadhi ya wadau wa mahakama wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango wakati wa ufunguzi wa Mjadala wa Tano wa Umoja wa Afrika unaohusu Mahakama leo Novemba 4,2021.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji wa mahakama kuu ya Tanzania kitengo cha Biashara, Dkt. Deo Nangela akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa Mjadala wa Tano wa Umoja wa Afrika unaohusu Mahakama leo Novemba 4,2021. Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere Dar es salaam.
Rais wa Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa Mjadala wa Tano wa Umoja wa Afrika unaohusu Mahakama leo Novemba 4,2021. Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere Dar es salaam.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wadau wa mahakama leo Novemba 4, 2021 wakati akifungua mkutano wa tano wa mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu na watu jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad