SERIKALI YAWAASA WAMILIKI WA VITUO VYA MAKUZI NA MALEZI WA WATOTO KUVISAJILI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 22, 2021

SERIKALI YAWAASA WAMILIKI WA VITUO VYA MAKUZI NA MALEZI WA WATOTO KUVISAJILI

Mratibu, Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto kutoka shirika la Anjita Child Development Foundation, Yasinta Mlay akisimamia Makundi ya wanaopewa mafunzo kwa watoto wachanga na watoto wadogo wakiendelea kufanya kazi walizopewa na mtoa mafunzo.
Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Lusajo Kafuko akizungumza na wamiliki na walezi katika vituo vya makuzi na malezi kwa watoto wachanga na watoto wadogo, mafunzo hayo yametolewa wilayani Mkuranga mkoani pwani.

KATIKA kuhakikisha watoto wanapata huduma za malezi na Makuzi kadili ya mwongozo na taratibu za serikali Shirika la Anjita Maendeleo kwa watoto limeendelea kutoa mafunzo kwa wamiliki na walezi wa watoto wachanga na watoto wadogo mchana.

Akizungumza na waandishi wa habari wilayani  Mkuranga Mkoani Pwani, Meneja Mradi wa Shirika la Anjia, Janeth Malela amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuongeza usajili wa vituo kwani kufanya hivyo kunaongezea thamani vituo hivyo.

Amesema kuwa kufanya usajili wa vituo vya kulelea watoto kutasaidia wa watoto hao kuwa katika mazingira salama na kuwa katika mazingira mazuri na ya kuvutia. 

Janeth amesema pamoja na watoto kuwa katika vituo vya malezi na Makuzi wanapata na kujifunza vitu vya msingi vya awali katika makuzi ya mtoto yanayohusiana na maendeleo ya mtoto kimwili, kiakili na lugha za mawasialiano.

Amesema kuwa Mafunzo hayo kwa Wamiliki na walenzi ni kwa wale wenye vituo vinavyolea watoto wa miaka 0 hadi 4 na miezi 11, watoto zaidi ya hapo wanatakiwa kuanza darasa la awali.

Mafunzo haya yanasaidia wamiliki na walezi kwajili ya kumatengenezea mazingira watoto wanapokuwa katika vituo vya malezi na na makuzi ili wawe katika mazingira salama, mazuri na yanayochangamsha kwenye ujifunzaji wa awali kimwili, kiakili na lugha za mawasiliano.

"Programu hii inaenda katika mikoa 10, kwa awamu ya kwanza tumeanza katika mikoa mitatu ambayo ni Rukwa, Mtwara na Pwani." Amesema Janeth.

Amesema mafunzo kama hayo yataanza tena mwakani 2022 hadi 2023 kwenye mikoa ya Lindi, Ruvuma, Iringa, Kagera na Kilimanjaro.

Mafunzo kwa wote program inawafikia kila wamiliki na walezi wa vituo katika kila mkoa na katika kila halmashauri.

Akizungumzia kuhusu serikali imejipangaje ili kuhakikisha mtoto anakuwa salama, Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Lusajo Kafuko amewaasa wamiliki wa vituo vya Malezi na makuzi kuvisajili Serikalini ili watambulike na shughuli zao zitambulike Serikalini.

Amesema usajili wa vituo hivyo ni bure kwani sheria ya mtoto namba 21 ya Mwaka 2009 kifungu cha 147 mpaka 152 na kanuni za watoto imetoa ufafanuai kuhusu vituo vya kulelea watoto wachanga na wadogo mchana na  imeeleza taratibu za kufuata wakati wa kufungua vituo vya makuzi na malezi kuwa na vigezo vinavyohitajika.

Amesema kuwa wilaya ya Mkuranga inavituo 123 vinavyojulikana na ustawi wa jamii kati ya hivyo vimesajiliwa vituo 21 tu.

Akitoa Mafunzo kwa miliki wa vituo na walezi wa watoto Mratibu, Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto kutoka shirika la Anjita Child Development Foundation, Yasinta Mlay amesema mafunzo hayo yamefanikiwa kwa sababu wamiliki na walezi wa vituo vya malezi na makuzi kwa mtoto wamefika kwa aslimia 90.

Amesema wamiliki na walezi wa watoto vituoni wamewawezesha ili waweze kufuata utaratibu uliowekwa na wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika kuendesha vituo vya malezi na makuzi na maendeleo ya Mtoto.

Amesema matarajio yao ni washiriki wa mafunzo hayo kuweza kufuata utaratibu uliowekwa na Serikali wa kuwachangamsha watoto na kuweza kupata maendeleo mhimu ya kiakili, kimwili, Lugha na mawasiliano, kijamii na kihisia.

Amesema kuwa Wamiliki na Walezi wa watoto wasiwafundishe watoto bali wawaelekeze kwa kutumia mbinu za ujifunzaji kupitia michezo mbalimbali.

"Hatutarajii kukuta kukuta ubao katika vituo vya makuzi na malezi kwa mtoto, tunatarajia kukuta Kadi za namba, herufi na vifaa mbalimbali vya michezo." Amesema Yasinta

Amesema kuwa Kupitia Mafunzo hayo walezi na wamiliki wa vituo hivyo wanaweza kutambua madhaifu na changamoto za mtoto akiwa bado mdogo na kutafutia uvumbuzi mapema inavyowezekana.

Kwa upande wa Mwakilishi wa walezi wa watoto ameiomba seikali kutoa mafunzo kama hayo nchi nzima ili wamiliki na viituo hivyo waweze kuvisajili vituo vyao kwa mwongozo wa serikali unavyosema.
Mratibu, Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto kutoka shirika la Anjita Child Development Foundation, Yasinta Mlay akitoa maelekezo kwa makundi wakati wa mafunzo ya Malezi na makuzi kwa watoto yaliyofanyika wilayani Mkuranga mKoani Pwani Novemba 20,2021.
Walezi wakifundishwa baadhi ya michezo ya watoto inayofuata sheria wakati wa mafunzo ya malezi na makuzi kwa wamiliki na walezi wa watoto wachanga na watoto wadogo.

Mmpoja wa walezi wa watoto akitoa moja ya mchezo wa kumpongeza mtoto ambapo amefanya vizuri (Mpasho) wakati wa mafunzo kwa walezi na wamiliki wa vituo vya malezi kwa watoto wachanga na watoto wadogo mchana.
Mazoezi yakiendelea kwa walezi na wamiliki wa vituo vya malezi na makuzi kwa watoto katika mafunzo yaliyofanyika wilayani Mkuranga Mkoani Pwani Novemba 20,2021.


Wawasilishaji wa makundi wakiwasilisha majibu ya maswali waliyopewa na Mkufunzi wao wakati wa mafunzo yaliyofanyika wilayani Mkuranga Mkoani Pwani Novemba 20,2021.

Picha mbalimbali katika makundi ya wamiliki na walezi wa watoto wachanga na watoto wadogo wakati wa mafunzo yaliyofanyika wilayani Mkuranga Mkoani Pwani Novemba 20,2021.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad