SERIKALI YAJIPANGA KUWANOA WAPIMA ARDHI TANZANIA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 25, 2021

SERIKALI YAJIPANGA KUWANOA WAPIMA ARDHI TANZANIA

Meza kuu.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi  (wa kwanza kulia) akipewa maelezo juu ya kifaa cha kupimia ardhi na Mpima Ardhi Degratias Karulama wa Kampuni ya Trade Investment.
Mpima Ardhi Msungu Daudi wa Kampuni ya Global Survey (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri Lukuvi akilezea jinsi vifaa vya kisasa vya upimaji wa ardhi vinavyofanya kazi.
Bwana Alfan Ngowo na Bi. Hellen wa Kampuni ya Esri Eastern Afrika wakitoa maelezo kwa Waziri Lukuvi.
Makamu wa Rais wa Taasisi ya Wapima Ardhi Tanzania IST, Bille Mussa akitoa hotuba yake.

Wanachama wa Taasisi ya Wapima Ardhi Tanzania IST wakifuatilia mkutano huo.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akitoa hotuba yake.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akitoa zawadi ya cheti kwa Mpima Ardhi wa muda mrefu.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/Michuzi Tv

Serikali imesema itaendelea kusimamia upangaji na uratibu wa kisheria katika matumizi ya ardhi nchini ili miongozo hiyo itoe huduma bora kwa wananchi pamoja na kumaliza migogoro ya ardhi ambayo imekua ikijitokeza kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Taasisi ya Wapima Ardhi Tanzania IST ambapo pamoja na mambo mengine amesema uwepo wa matumizi sahihi wa Sheria ya ardhi mbali na kusaidia kuweka usawa kwa wamiliki utasaidia pia migogoro ya hapa na pale.

Waziri Lukuvi amesisitiza kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wapima ardhi ambao watabainika kufanya kazi zao bila kufuata sheria na taratibu za kazi yao kwa maslai binafsi.

Amesisitiza umuhimu kwa wana taaluma hao kujitangaza wenyewe ili kufuta sifa mbaya iliyopo miongoni mwa Watanzania kuhusu utendaji kazi wao. Amesema sifa mbaya inasambaa zaidi kuliko utendaji kazi bora wa IST ambao unafanywa siri.

Lukuvi amesema hatua hiyo itasaidia, kuondoa dhana potofu iliyojengeka kwa wananchi kuwa IST ni walanguzi au wapimaji ni watu waharibifu na kwamba watanzania wataona kazi nzuri inayofanywa chama hicho.

“Bado wana dhana ya kwamba ukimkuta mpima ardhi basi ni yule anayepima mara mbili. Imezoeleka zamani eneo moja linapimwa mara mbili, lakini hatuja wao kuona kazi nzuri inayofanywa na wapima ardhi na ramani.

Ameongeza kuwa wapo wapima ardhi na ramani walioshiriki na kufanya vizuri katika miradi mbalimbali ikiwemo ya bomba la mafuta, barabara, mradi wa kusambaza umeme vijijini, lakini hawajahi kuonekana au kutambuliwa na wananchi wa maeneo mbalimbali.

“Nimewaambia viongozi wenu wajenge utaratibu wa kuratibu shughuli zinazotekelezwa na mwanachama mmoja mmoja ili Watanzania wazijue. Watanzania walio wengi wanajua nyinyi ni walanguzi tu hasa wale wa halmashauri,” alisema.

 “Tengenezeni mtandao wenu, sasa hivi watu wanasoma sana na muweke utaratibu wa kila mwanachama akiwa kazini atume picha ya namna anavyotekeleza majukumu yake ili ikifika siku kama ya leo  watu waone kazi  bora zilizofanywa kwa mwaka huu. Lazima mjisafishe watu waone kuna kazi nzuri mnafanya.

“Vinginevyo mtabaki na kashfa zenu kuwa ni walanguzi, uko nje tuna wajua bahati mbaya sekta yangu kila mmoja ana sehemu yake mbaya ambayo haijafutika.Maofisa mipango miji wana sifa zao wanaweza kubadilisha hata eneo la makaburi kuwa kituo cha mafuta, ndipo wanapokula wao,” alisema Lukuvi.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa IST, Bille Mussa ameiomba Serikali kuzifanyia marekebisho ya baadhi ya sheria za ardhi ili ziendane na wakati na kuifanya Sekta hiyo kutoa huduma zake kwa ufanisi kwaajili ya maslai ya wapima ardhi na Taifa kwa Ujumla.

Amesema mkutano huo, una malengo mbalimbali kiujadili changamoto mbalimbali za kitaalamu wanazokutana nazo kwa nyakati tofauti katika shughuli zao za kila siku.

Lengo jingine ni pamoja na kukumbushana wajibu na nidhamu ya kazi kwa anachama wao kuhusu utoaji huduma kwa wananchi. 

“Pia tutajadili kwa pamoja mabadiliko ya teknolojia na changamoto kwa wana taaluma na kuweka mikakati ya namna kukabiliana nazo. Pia tutajadili namna taaluma ya upimaji ardhi na ramani inavyoshiriki katika utekelezaji wa mkakati wa maendeleo endelevu ya nchi”

Kila mwaka Taasisi ya Wapima Ardhi Tanzania IST hufanya Mkutano Mkuu kwaajili ya kujadili masuala mbalimbali ambapo kwa mwaka 2021 mkutano huo unakwenda na Kauli mbiu isemayo " Jukumu la Taaluma ya Upimaji na Ramani katika ujenzi wa Miundombinu na Maendeleo Endelevu Tanzania.

3 comments:

  1. Zipo changamoto na sababu zinazoonesha wapima ardhi kama walanguzi, na nadhani hujadiliwa kila mwaka ila utekelezaji wake huwa mdogo sana... Udhaifu nadhan upo pande zote, IST na serikali lakini pia kuna hii inaitwa NCPS

    ReplyDelete
  2. Ukosefu wa standards za utendaji kazi wa wapima hasa katika kutoa huduma za upimaji pamoja na maadili ya kazi (ethics) hupelekeaa kuonekana kama taaluma yenye kudharaulika. kuonekana kama taaluma yenye kudharaulika. Nafikirk IST waje n mpango wa kutengeneza viwango vya utendaji wa wapima pamoja na kufuatilia maadili ya kazi katika kazi mbalimbali wanazozifanya.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad