HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 1, 2021

REA watembelea miradi ya umeme vijijini mkoani Njombe

 Na Amiri Kilagalila,Njombe

ILI kuendelea na jitihada za kuwafikishia nishati ya umeme wananchi hususani wa vijijini,wateja 120 wanatarajiwa kuunganishiwa huduma ya umeme kupitia kampuni ya Matembwe Village Company inayosimamia mtambo wa kuzalisha umeme kwa maporomoko ya maji uliopo katika kijiji cha Ikondo wilayani Njombe.

Advera Mwijage ni kaimu mkurugenzi wa uendelezaji masoko na teknolojia kutoka wakala wa nishati vijijini (REA) amebainisha hilo wakati wa ziara ya uongozi wa wakala wa nishati vijijini pamoja na mkurugenzi mkuu walipotembelea katika mradi huo pamoja na miradi mingine mkoani Njombe inayozalisha umeme kwa maporomoko ya maji.

“Serikali tumechangia milioni 700 katika mradi huu kwa ajili ya kuunga wateja 586 na katika mradi wetu ambao tunaendelea nao kupitia ufadhili wa SIDA wataongezewa wateja 120 watakao kuwa kwenye vijiji 8,kupitia ziara hii wataweza kuongeza hao wateja ili wananchi wengi zaidi waweze kupata huduma”alisema Advera Mwijage

Mwijage amesema wakala wa nishati vijijini kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanawawezesha wawekezaji wadogo ili kuwasaidia kusambaza umeme katika maeneo ya vijiji ambavyo vinaweza kuchelewa kupata nishati kwa kusubiri wakala huyo.

Vilgilio Kihwele ni fundi mkuu wa mitambo hiyo ya uzalishaji umeme,amesema mradi huo huzalisha takribani kilowati 550 ambazo huongezwa nguvu na kuzalisha vote zaidi ya 1000 na hivyo kufikia matumizi ya nishati kwa 60% pekee.

“Katika mradi huu tunahudumia vijiji nane kwa hiyo ile ziada baada ya kuhudumia kwenye vijiji vyote inakwenda TANESCO,na kwa matumizi yetu kwa sasa tupo kama kama 60% na hiyo ziada yote inayobaki inakwenda TANESCO”Alisema Vilgilio Kihwele

Kwa upande wake Johanes Kamonga ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Matembwe Village Company Limited inayosimamia mradi huo wa uzalishaji umeme amesema,watahakikisha wanasimamia kikamilifu mradi ili uendelee kuzalisha umeme.

“Tunawahakikishi wananchi kupata nishati endelevu kwa kusimamia mtambo uwe salama,uzalishe umeme wa viwango lakini pia tutatoa huduma kwa kila kijiji kwa kupeleka wataaalamu ili kupita kwa wateja kujua kila changamoto”alisema Kamonga

Zaidi ya vijiji 8 vinanufaika na mradi huo huku wananchi wanaoishi karibu na mradi na kuunganishiwa umeme wakifanikiwa kutumia nishati hiyo katika shughuli mbali mbali ikiwemo kuanzisha viwanda vidogo vidogo na kuboresha hali ya maisha yao.

Baadhi ya viongozi kutoka wakala wa nishati vijijini na wasimami wa mradi wa umeme wa maji Ikondo wakikagua na kupata maelekezo jinsi mradi huo unavyofanya kazi.
Vilgilio Kihwele ni fundi mkuu wa mitambo hiyo akitoa baadhi ya maelekezo kwa mkurugenzi mkuu wa wakala wa nishati vijiji (REA) alipotembelea mtambo wa kuzalisha umeme kwa maporomoka ya maji uliopo kijiji cha Ikondo wilayani Njombe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad