MWIGULU MGENI RASMI KONGAMANO LA 12 LA MWAKA LA WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 8, 2021

MWIGULU MGENI RASMI KONGAMANO LA 12 LA MWAKA LA WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI

Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imeandaa kongamano la 12 litakalowakutanisha wataalam hao  lengo la kujadili ubunifu wenye suluhisho katika utekelezaji wa Ununuzi na Ugavi kwa kutambua ushindani na mapinduzi ya Viwanda kwa maendeleo ya Jamii.

Akizungumza Jijini Dar  es salaam Kaimu Mkurugenzi Matendaji wa bodi  hiyo, Godfred Mbanyi   amesema kongamano hilo linatarajiwa kuanza Novemba 30 hadi Desemba 03 mwaka 2021 na litafanyika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha(AICC). Hivyo kawaasa waalikwa wa kongamano hilo kwenda na wakati ili kuongeza ufanisi katika kongamano hilo.

Mbanyi amesema katika Kongamano hilo Wataalamu hao watapata nafasi ya kujadili, kuchambua, kuweka mikakati ya uboreshaji katika Sekta ya Ununuzi na Ugavi katika Ununuzi wa Umma na Kampuni Binafsi inayoendana na Sekta ya viwanda ili kuweza kuongeza ajira kwa wananchi hasa kwa wenye fani ya Ununuzi na Ugavi.

“Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kongamano la 12 la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi anatarajiwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba.

 ''Nawaomba sana wataalamu, wadau  na watu wote wenye nia ya kutambua mchango wa fani hii katika maendeleo ya Viwanda wajitokeze pale Arusha kuanzia terehe 30 Novemba mwaka huu” alisema Mbanyi

Amesema Bodi hiyo imeandaa wataalamu katika mada mbalimbali watakaochanganya nadharia na vitendo kwa washiriki watakaokuwa kwenye kongamano ili waweze kupta mapana katika masuala ya Ununuzi na Ugavi kwa namna gani yanaweza kuchangia mapinduzi ya Viwanda na hatimae kuleta maendeleo katika nchi.

“Watu wote wanaotaka kushiriki Kongamano hili wafuate maelekezo yaliyowekwa kwenye Tovuti ya Bodi hiyo pamoja na mitandao ya kijamii ya Bodi na pia waakikishe wamefanya malipo yao mapema kabla ya Novemba 30 mwaka huu ili kuondoa usumbufu wakati wa Kongamano hilo”. Alisema Mbanyi
 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kongamano la 12 la wataalamu wa Ununuzi na Ugavi litakalowakutanisha wataalam hao kwa lengo la kujadili ubunifu wenye suluhisho katika utekelezaji wa Ununuzi na Ugavi kwa kutambua ushindani na mapinduzi ya Viwanda kwa maendeleo ya Jamii litakalofanyika jijini Arusha kuanzia Novemba 30 hadi Desemba 03, 2021.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi(katikati aliyekaa)  akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto aliyekaa ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa PSPTB, Paul Bilabaye(kushoto) pamoja na  kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini Tanzania(PSPTB), Amos Mang’ombe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad